Leo hii Uwanja wa Etihad Jijini
Manchester utalipuka kwa mpambano mkali wa Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Mtoano
ya Timu 16 ya UEFA CHAMPIONZ LIGI kati ya Manchester City na FC Barcelona.
Mechi hii ni Marudio ya Mechi
ya Msimu uliopita ya Raundi hii hii ya Mashindano haya wakati Man City
ilipotolewa na Barcelona kwa Jumla ya Mabao 4-1 katika Mechi mbili ambazo kila
Mechi City ilimaliza Mtu 10 baada ya Mchezaji wao mmoja kupewa Kadi Nyekundu.
kwenye Marudiano huko Nou Camp,
Barca ilishinda Bao 2-1.
Man City itamkosa Kiungo wao
mahiri Yaya Toure ambae anamalizia Kifungo chake cha Mechi 3 alichopewa na UEFA
lakini Straika wao mpya Wilfried Bony ruksa kuanza Mechi hii.
Barcelona huenda wakamchezesha
Straika wao Luis Suarez ambae atakuwa akicheza Mechi yake ya kwanza Nchini
England tangu aihame Liverpool mwanzoni mwa Msimu.
Akiongelea mtanange huu wa Uwanja wa Etihad, Sentahafu wa Barca,
Gerard Pique, ambae aliichezea Man United ambao ni Mahasimu wakuwa wa City,
alisema: “Hii ni moja ya Gemu ya Mwaka, na ni muhimu kwetu kwa sasa. Watajaribu
kutushambulia na hilo linatufaa sisi. Imedhihirishwa kwamba tunakuwa vyema
dhidi ya Timu zinazotushambulia kwa sababu tunaweza kupiga kaunta ataki!”
Nae Straika wa Man City, Sergio
Aguero, ametamka: “Hii ni Gemu mpya na sisi sasa si sawa na Msimu uliopita na
wao pia sivyo!”
Meneja wa City Manuel
Pellegrini ameahidi Timu yake itacheza kwa kushambulia tu.
MECHI NYINGINE LEO
Juventus FC vs BV Borussia Dortmund
0 comments:
Post a Comment