BAO la Dakika ya 82 la Paul Pogba limewapa ushindi wa Bao 1-0 Mabingwa Watetezi Juventus walipoichapa Sassuolo Bao 1-0 kwenye Mechi ya Ligi Serie A Uwanjani Juventus Arena Jijini Turi huko Italy na kuwapaisha Juve Pointi 11 mbele kileleni mwa Ligi hiyo.
Jumapili, AS Roma, Timu ya Pili kwenye Msimamo wa Serie A, ilitoka Sare 0-0 Ugenini na Chievo Verona katika Mechi iliyochezwa huko Stadio Marc'Antonio Bentegodi Mjini Verona.
SOURCE: SOKA IN TANZANIA
0 comments:
Post a Comment