Pages

Friday, 6 March 2015

TAIFA STARS KUCHEZA NA MALAWI CCM KIRUMBA , REFA MTANZANIA KUCHEZESHA MECHI YA KIMATAIFA

Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) itashuka dimbani jumapili Machi 29 mwaka huu, kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya Taifa ya Malawi (The Flames) katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Mchezo huo wa kirafiki ambao upo katika kalenda ya FIFA kwa timu za Taifa (Machi 23-31) na utatarajiwa kuanza majira ya saa 10 na nusu jioni kwa saa za Afrika Mashariki.
 
MTANZANIA KUCHEZESHA MECHI YA ZESCO NA KALOUM 
Mwamuzi wa kimataifa wa Tanzania mwenye beji ya Fifa, Israel Mjuni Nkongo amechaguliwa kuchezesha mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya wenyeji Zesco FC ya Zambia dhidi ya AS Kaloum ya Guinea.
Katika mchezo huo wa kwanza wa mzunguko wa pili, Nkongo atasaidiwa na washika kibendera John Kanyenye na Josephat Bulali na mwamuzi wa akiba Waziri Sheha wote kutoka Tanzania, huku Kamisaa wa mchezo akiwa Mayixole Elvin Shishana kutoka nchini Afrika Kusini 
Mchezo huo unatarajiwa kufanyika kati ya tarehe 13,14,15 Machi mwaka huu nchini Zambia

Share:

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

IDADI YA WANAOTEMBELEA BLOG HII

Blog Archive

Recent Posts

Fashion

3/Fashion/big-col-right

Recent Posts

Header Ads

Followers

Powered By Blogger

Tags

Maoni

3/recent-comments

WASILIANA NASI

Popular Posts

Labels

Blog Archive

Blogger templates