Goodison Park umeendelea kuwa Uwanja mbaya kwa Man United baada hii Leo kutandikwa Bao 3-0 na Everton katika Mechi ya Ligi Kuu England.
Kwa Miaka ya hivi karibuni Goodison Park pamekuwa pagumu kwa Man United ambako wameshinda Mechi 1 tu katika Mechi zao 7 zilizopita na kutoka Sare 2 na kufungwa 4 na hii ni mara ya 3 mfululizo kufungwa hapo.
Hii Leo Man United walikuwa nyuma kwa Bao katika Dakika ya 5 baada ya James McCarthy kumalizia kaunta ataki safi na Dakika ya 35 wakapigwa tena Bao la Pili baada ya kona kumaliziwa na John Stones.
Kipindi cha Pili Dakika ya 74 Kevin Mirallas aliifungia Everton Bao la 3 wakati Difensi ya Man United ikidhani Mpira utasimamishwa kwa Ofsaidi.
Matokeo haya yamewabakisha Man United Nafasi ya 4 wakiwa Pointi 7 mbele ya Timu ya 5 Liverpool ambao wana Mechi 1 mkononi.
0 comments:
Post a Comment