Pages

Friday, 29 May 2015

HABARI ZA USAJILI TANZANIA LEO KUBWA MUSSA HASSANI MGOSI AREJEA TENA SIMBA ASAINI MKATABA

SIMBA SC imemsajili tena mshambuiaji wake wa zamani, Mussa Hassan Mgosi leo hii, baada ya takriban misimu miwili mizuri akiwa na Mtibwa Sugar ya Morogoro.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amesema mjini Dar es Salaam kwamba wamemrejesha Mgosi kikosini baada ya kuvutiwa na juhudi zake akiwa Mtibwa.

*********************************
Klabu ya Mtibwa Sugar imeweka wazi msimamo wake kuwa ipo tayari kuwapokea wachezaji wake wote wa zamani ambao wanahitaji kurejea klabuni hapo, isipokuwa Shabani Kisiga kutokana na kuwa na rekodi mbaya ya nidhamu.
Kuna taarifa kuwa huenda wachezaji hao wakiwemo Hussein Javu, Nizar Khalfan wa (Yanga), Hussein Sharif ‘Cassilas’, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’ (Simba) wanaweza kurejea klabuni hapo.
***********************
SIMBA SC imesajili mabeki wawili wa Kizanzibari, Samir Hajji Nuhu wa kushoto na Mohammed Fakhi wa kati usiku wa leo.
Nuhu alikuwa mchezaji wa Azam FC kwa misimu miwili hadi msimu wa 2013/2014 kabla ya kuumia goti na kuondolewa katika usajili, wakati Fakhi msimu huu amechezea JKT Ruvu.
Mabeki hao vijana wadogo wamesaini leo mikataba ya kuitumikia Simba SC, Nuhu mwaka mmoja na Fakhi miaka miwili.
Share:

Tuesday, 26 May 2015

TAARIFA ZA USAJILI BONGO LEO KUBWA YANGA YAMSAINISHA KINDA WA KMKM HUKO SIMBA NDEMLA ASAINI MIAKA MITATU

Simba imekata mzizi wa fitna baada ya kumpa mkataba wa miaka mitatu mingine kiungo wake Said Ndemla shughuli iliyofanyika jijini Dar es Salaam, leo.
Ndemla amesaini mkataba wa miaka mitatu mingine kuendelea kuichezea Simba ambayo amekuwa akiitumikia kama mchezaji kinda.Awali kulikuwa na taarifa za Ndemla kuwaniwa na Yanga baada ya kusikia amebakiza mwaka mmoja tu na Simba.Lakini Msimbazi, wameifuta ndoto hiyo baada ya kuhakikisha Ndemla anaendelea kubaki Msimbazi zaidi na zaidi.
*****************Yanga imefanikiwa kumsajili beki Haji Mwinyi kutoka KMKM ya Zanzibar.Haji Mwinyi amesaini kuichezea Yanga leo na sasa yuko njiani kurejea kwa Zanzibar.“Kweli Haji amesaini Yanga leo, ataichezea kwa miaka miwili na kila kitu kimeisha.“Tuko njiani tunarejea Zanzibar, shughuli zote zimefanyika kwenye makao makuu ya Yanga,” kilieleza chanzo.Mwinyi alikuwa katika kikosi cha Taifa Stars kilichoshiriki michuano ya Kombe la Cosafa nchini Afrika Kusini.

******************
Pamoja na Mwinyi, Yanga imefanikiwa kumnasa kipa wa Kagera Sugar, Benedicto Tinocco.
Tinocco licha ya kuwa tegemeo katika kikosi cha timu ya taifa ya vijana, pia aliwahi kuwa kipa bora wa michuano ya Copa Coca Cola.


Share:

KOCHA WA HISPANIA ATAJA KIKOSI DIEGO COSTA HAYUPO

Kocha wa Spain Vicente del Bosque amewaita Vijana wapya wawili wa Sevilla, Sergio Rico na Aleix Vidal, kwa ajili ya Mechi zao za Juni dhidi ya Costa Rica na Belarus na kumwacha Straika wa Chelsea Diego Costa.
Kipa Rico, Miaka 21, na Winga Vidal, Miaka 25, wamekuwa waking'ara Msimu huu na Sevilla ambayo imemaliza La Liga ikiwa Nafasi ya 5 na Jumatano Mei 27 huko Stadion Narodowy Mjini Warsaw, Poland, watacheza na Klabu ya Ukraine Dnipro Dnipropetrovsk kwenye Fainali ya Europa Ligi.
Wachezaji hao wawili wanaungana na mwenzao wa Sevilla, Vitolo, kwenye Kikosi cha Wachezaji 24 wa Spain.
Spain watacheza Mechi ya Kirafiki na Costa Rica huko Jijini Leon, Spain hapo Juni 11 na Juni 14 kucheza Ugenini huko Borisov na Belarus kwenye Mechi ya Kundi lao la EURO 2016.

KIKOSI KAMILI CHA SPAIN:
De Gea (Manchester United), Casillas (Real Madrid), Rico (Sevilla); Alba (Barcelona), Bartra (Barcelona), Bernat (Bayern), Carvajal (Real Madrid), Juanfran (Atlético Madrid), Pique (Barcelona), Ramos (Real Madrid), San José (Athletic Bilbao); Busquets (Barcelona), Cazorla (Arsenal), Fàbregas (Chelsea), Iniesta (Barcelona), Isco (Real Madrid), Koke (Atlético Madrid), Pedro (Barcelona), Silva (Manchester City), Vidal (Sevilla), Vitolo (Sevilla); Alcacer (Valencia), Morata (Juventus), Nolito (Celta Vigo).
Share:

KIKOSI CHA TANZANIA KITAKACHOWAVAA MISRI HIKI HAPA KESHO KUINGIA KAMBINI


Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inatarajiwa kuingia kambini kesho jumatano katika hoteli ya Tansoma iliyopo eneo la Gerezani jijini Dar es salaam kujiandaa na mchezo dhidi ya Misri kuwania kufuzu kwa AFCON.
Kocha Mkuu wa Taifa Stars Mart Nooij, amewaita wachezaji 16 kuingia kambini kesho siku ya jumatano kwa ajili ya kupimwa afya zao na kujua maandeleo yao kabla ya kuwajumisha katika kikosi cha pamoja kitakachokua kwenye maandalizi ya mchezo dhidi ya Misri.

Wachezaji walioitwa kuingia kambini kesho ni, Mohamed Hussein, Peter Manyika, Hassan Isihaka, Jonas Mkude (Simba SC), Salum Telela, Juma Abdul, Nadir Haroub (Yanga SC), Aishi Manula, Mudathir Yahya, Frank Domayo, Kelvin Friday (Azam FC), Rashid Mandawa, Atupele Green (Kagera Sugar), Haroun Chanongo (Stand United) Malimi Busungu (Mgambo JKT) na Emmanuel Simwanda (African Lyon).
Mara baada ya kurejea kutoka nchini Afrika Kusini, kocha wa Stars Nooij aliwapa mapumziko ya siku 10, wachezaji waliokua kwenye michuano ya Cosafa mpaka Juni Mosi ambapo ndipo watajumuika na wachezaji wengine waliopo kambini.

Ifikapo Juni Mosi, 2015 Taifa Stars itaanza kambi ya moja kwa moja kujiandaa na mechi dhidi ya Misri itakayochezwa jijini Alexandria katika uwanja wa Borg El Arab Juni 14, 2015 ikiwajumuisha pia wachezaji Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wanaocheza soka la kulipwa katika klabu ya TP Mazembe ya Congo DR.
Kabla ya kuelekea nchini Misri, Taifa Stars inatarajiwa kuweka kambi jijini Addis Ababa nchini Ethiopia kuanzia tarehe 4,Juni 2015 kwa muda wa wiki moja kabla ya kuelekea nchini Misri kwenye mchezo huo dhidi ya Mafarao.
Share:

REAL MADRID YAMTIMUA RASMI CARLO ANCELOTTI HUWENDA RAFAEL BENITEZ AKACHUKUA MIKOBA


Carlo Ancelotti ametimuliwa kama Kocha wa Real Madrid baada ya kuiongoza kwa Misimu Miwili na kuiwezesha kutwaa UEFA CHAMPIONZ LIGI kwa mara ya 10.
Ancelotti, Raia wa Italy mwenye Miaka 55 ambae Mkataba wake na Real ulitakiwa kwisha mwishoni mwa Msimu ujao, Msimu uliopita alileta mafanikio Klabuni hapo kwa kutwaa UEFA
CHAMPIONZ LIGI na Copa del Rey na kisha kutwaa Kombe la Klabu Bingwa Duniani lakini Msimu huu wametoka kapa bila Kombe.

Mafanikio pekee ya Real Msimu huu ni toka kwa Mchezaji wao Bora Duniani, Cristiano Ronaldo, ya kutwaa Pichichi, Tuzo ya Mfungaji Bora La Liga huku Ubingwa wa Ligi hiyo ukienda kwa Mahasimu wao Barcelona.
Msimu huu, Real walishindwa kutetea Taji lao la UEFA CHAMPIONZ LIGI baada ya kutolewa Nusu Fainali na Juventus ambao sasa watacheza Fainali na Barcelona hapo Juni 6.
Kwenye Copa del Rey walibwagwa nje na Atletico Madrid ambao nao walitupwa nje na Barca ambao Wikiendi hii watacheza Fainali na Athletic Bilbao.
Kwenye La Liga, Kikosi cha Ancelotti kimemaliza Nafasi ya Pili, Pointi 2 nyuma ya Mabingwa Barcelona.
Akitangaza uamuzi wa kumwondoa Carlo Ancelotti, Rais wa Real, Florentino Perez, alisema Jana: "Nini Ancelotti alikosea? Sijui. Ila Klabu hii inadai mambo makubwa. Mapenzi ya Wachezaji na Washabiki kwa Carlo ni makubwa kama vile kwangu kwake!"
Perez ameahidi kutangaza Kocha mpya Wiki ijayo huku Mhispania Rafael Benitez akitajwa sana kuwa mrithi
.
Share:

Monday, 25 May 2015

BRENDAN ROGERS ASEMA HATOKI LIVERPOOL MBALI NA LIVERPOOL KUCHEZEA KIPIGO CHA 6-1


Huku Mashabiki wakipandwa na jazba kwa Timu yao kubamizwa Bao 6-1 na Stoke City hapo Jana, Meneja wao Brendan Rodgers amesema ataondoka Liverpool ikiwa Wamiliki wake watataka hilo.
Jana huko Britannia Stadium Liverpool waliaaga Msimu wa Ligi Kuu England kwa kichapo hicho cha Bao 6 na pia kumuaga Kepteni wao Steven Gerrard ambae anaondoka kwenda kumalizia Soka lake huko Marekani.

Rodgers amekiri kuwa yuko kwenye presha kubwa baada ya kushinda Mechi 2 tu katika 9 zilizopita na kumaliza Nafasi ya 6 kwenye Ligi ikimaanisha Msimu ujao watacheza UEFA EUROPA LIGI.

Pia Rodgers amekiri ni fedheha kwa Timu yao kupigwa Bao 6 kitu ambacho hakijatokea kwao kwa Miaka 52 na kuwaomba radhi Mashabiki wao.
Katika Mechi hiyo Brendan Rodgers alimpiga benchi Staa wao Raheem Sterling ambae amegoma kusaini Mkataba mpya na kung'ang'ania kuhama.
Hadi Mapumziko Liverpool ilikuwa nyuma kwa Bao 5-0 zilizofungwa ndani ya Dakika 23 na Mame Biram Diouf, Bao 2, Jonathan Walters, Charlie Adam na Steven N'Zonzi.
Bao pekee la Liverpool lilifungwa na Steven Gerrard katika Kipindi cha Pili ambacho pia Stoke walipiga Bao lao la 6 kupitia Peter Crouch.
Share:

TFF YASHINDWA KUMTIMUA MART NOOIJ KUINOA TAIFA STARZ APEWA MASHARTI YA KUFUZU CHAN

Kamati ya utendaji ya TFF imesikitishwa na mwenendo mbovu wa Taifa Stars Rais wa TFF, Jamal Malinzi kwa niaba ya kamati ya utendaji amewaomba radhi wapenzi wa mpira kwa matokeo mabaya ya Taifa Stars kwenye michuano ya Cosafa.
Kikao cha kamati ya utendaji kilipokea taarifa juu ya mwenendo wa timu ya Taifa.
Baada ya majadiliano ya kina, ilikubaliwa kuwa kocha mkuu wa timu ya Taifa, Mart Nooij apewe changamoto maalumu ya kufuzu kwa fainali za Afrika kwa wachezaji wa ndani CHAN na asipofanikisha jambo hilo mkataba wake utasitishwa mara moja.
Maamuzi haya yamezingatia hali halisi ya timu ya Taifa ambayo inakabiliwa na michuano mbalimbali ya kimataifa ndani ya kipindi kifupi.
Aidha katika kuliimarisha benchi la ufundi la timu ya Taifa, Leopald Tasso Mkebezi ameteuliwa kuwa meneja mpya wa timu ya Taifa.
Mkebezi amewahi kuwa meneja wa timu ya Taifa katika kipindi cha mwaka 2006 - 2012.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
Share:

Sunday, 24 May 2015

UMEWAHI KUWAONA MAYWEATHER NA MANY PAC WABONGO? HEBU CHEKI HAWA WATOTO WATANZANIA WALIVYOZICHAPA


Chipukizi Salim Mponda akipiga ngumi ya kuingia ndani mwenzake Hemed Mrema wakati wa mpambano wa shoo uliofanyika katika ukumbi wa Panandi Panandi Jumamosi 
Mwenyekiti wa kamisheni ya ngumi za kulipwa (TPBC) Chaurembo Palasa kushoto akimkabidhi mtoto Salim Mponda kifuta jasho ambacho kilitolewa na mashabiki wa mchezo wa masumbwi yaliyofanyika jumamosi katika ukumbi wa Panandi Panandi, ilala baada ya kuonesha shoo safi ya ngumi.
Picha zote na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Share:

TETESI ZA USAJILI HAPA BONGO LEO KUBWA NIA DEUS KASEKE NA HARUNA CHANONGO WATUA JANGWANI

Kiungo nyota aliyetamba na Mbeya City, Deus Kaseke sasa ni mali ya Yanga.
KAseke amejiunga baada ya kuingia mkataba wa kuichezea timu hiyo jana.
Mabingwa hao walikuwa wakipambana kuimarisha kikosi chao kwa ajili ya michuano ya kimataifa.
KAseke amejiunga na Yanga baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili, jana.
Taarifa kutoka ndani ya Yanga zimeeleza, Kaseke amemaliza na uongozi wa Yanga jana, hivyo sasa ni mali ya Jangwani.

*******************
Baada ya tetesi za muda mrefu, hatimaye mambo yameamilika baada ya Yanga kufanikiwa kumsajili kiungo Haruna Chanongo.
Yanga imemsajili Chanongo akitokea Simba ambayo ilikuwa imepeleka Stand United kwa mkopo.
Suala la usajili wa Chanongo limekamilika jana kwa mkataba wa miaka miwili na sasa ni mchezaji halali wa Yanga.


Share:

JURGEN KLOPP AAGWA KWA SHANGWE SIGNAL IDUNA PARK HUKU TIMU HIYO IKICHINDA 3-2 DHIDI YA WERDER BREMEN

Kocha wa Borussia Dortmund Jurgen Klopp Leo ameagwa kwa mtindo wa kuvutia Uwanjani Signal Iduna Park katika Mechi yao ya mwisho ya Bundesliga Msimu huu wakati Timu yao ilipoichapa Werder Bremen Bao 3-2.
Kabla ya Mechi hiyo kuanza, Washabiki waliinua Bango kubwa lenye Picha ya Klopp na Maandishi 'DANKE JURGEN' yakimaanisha 'Asante Jurgen'.

Jurgen Klopp alishatangaza mapema kuondoka Klabuni hapo mwishoni mwa Msimu huu na huenda akaondoka na kuwaachia Kombe kwani Wikiendi ijayo Jumamosi Mei 30, Dortmund itacheza Fainali ya Kombe la Germany, DFB-Pokal, dhidi ya VfL Wolfsburg.
Share:

MECHI ZA MWISHO ZA LA LIGA UTAMU TUPU RONALDO MFUNGAJI BORA ATUPIA HETRIKI NAE MESSI ATUPIA MBILI HUKU LEGENDARY XAVI AKIAAGWA

Msimu huu wa La Liga ulifungwa rasmi Jana.

Huko Nou Camp Mabingwa Barcelona walishuhudia Kiungo wao Mkongwe Xavi mwenye Miaka 35 akicheza Mechi yake ya mwisho ya La Liga kwani anastaafu na kwenda kucheza huko Qatar.
Xavi aliichezea Barca kwa Miaka 24.
Lakini katika Mechi hii licha ya Barca kutangulia 2-0 kwa Bao za Messi Deportivo La Coruna walicharuka na kurudisha Bao zote kupitia Perez Martinez na Salomao na kupata sare ys 2-2.
***************************
Huko Santiago Bernabeu, Real Madrid, ambayo imemaliza Msimu ikiwa ya Pili nyuma ya Barca, iliifumua Getafe Bao 7-3.
Bao za Real zilifungwa na Ronaldo, Bao 3, Chicharito, James Rodriguez, Jese Rodriguez na Marcelo.

Kwenye Mechi hii Ronaldo alipumzishwa katika Dakika ya 58 na nafasi yake kuchukuliwa na Kinda kutoja Norway, Martin Odegaard, alieweka rekodi ya kuwa Mchezaji alie na umri mdogo kuichezea Real akiwa na Miaka 16, Miezi 5 na Siku 6.
RONALDO-KINDAODEGAARD
Kinda huyo alijiunga na Real Mwezi Januari akitokea Klabu ya Norway Stromsgodset.
Share:

Saturday, 23 May 2015

DONDO ZA USAJILI KWA MUJIBU WA MAGAZETI MBALI MBALI ULAYA KUBWA PETR CECH

THE SUN
Stoke City wamemuandikia Begovic mkataba mpya ila kocha wa Stoke City Mark Hughes amesema uwamuzi wa kipa huyo kubaki uko kwenye maamuzi yake
**********
DAILY EXPRESS
Kiungo wa Hull City Jack Livermore atafukuzwa klabuni hapo baada ya kugundulika anatumia cocaine kwa mujibu wa vipimo anavyo fanyiwa klabun apo
******************
Manchester United inawataka wachezaji wawili wa Roma Miralem Pjanic 25, na Radja Nannggolan 27 na watagharimu kiasi cha €66 million
*********************
Liverpool inataka kumsajiri mchezaji wa Juventus Andre Pirlo kama ataamua kuondoka klabuni hapo mwisho wa msimu
Pirlo 35 anaweza kuondoka Juventus kwa tetesi ya kwamba Xabi Alonso Atajiunga na Juventus

DAILY MAIL
West Ham wameamuo kuonyesha nia ya kumsain kocha wa Napoli kwa sasa Rafa Benitez kwa mujibu wa klabu iyo kuwa Benitez ndo anaongoza katika list yao ya makocha wanao wataka

Mmiliki wa Hull City Kocha wa Timu hiyo Steve Bruce ataendelea kuifundisha timu yake hata kama itashuka daraja

THE GURDIAN
Kiungo wa Athletico Madrid Koke amesema hata ihama klabu yake kwa msimu wara utakao kuja licha ya kuwa na tetesi kuwa mchezaji huyo anampango wa kujiunga na Chelsea
****************
Kiungo wa Everton Kevin Mirallas amesema anafulaha akiwa klabun hapo

THE INDEPENDENT
kocha wa Man City Manueli Pellegrin amesisitiza kuwa mshambuliaji wake raiwa wa Argentina Sergio Aguero hata ondoka klabuni hapo licha ya Real Madrid kumuwinda vikali mchezaji huyo

DAILY STAR
Kocha wa Man United amesema gori kipa wake David De Gea ni mda wa kuonge kama atabakia klabuni hapo au atakwenda Real Madrid ya Hispain
****************
Kocha Manueli Pellegrin amesema kibarua chake hakina wasi na ndo maana haina haja ya kukutana na wamiliki
****************
Dick Advocact ataendelea kuinoa sunderland mpaka msimu Ujao
Kocha Arsena Wenger amesema Kama timu yake wachezaji hawata onyesha kiwango atawaweka sokon majira ya joto
********************
Arsenal, Liverpool na Manchester United zinamuwania forwad wa Real Madrid Karim Benzema
Real Madrid wamesema timu moja kati ya hizo inaweza kumpata mchezaji huyo ili kumpisha Alvaro Morata kutoka Juventus
******************
DAILY TELEGRAPHY
Kipa wa Chelsea Peter Cech atajiunga na Man Utd endapo De Gea atakwenda Real Madrid
****************
Kocha wa Manchester United kwa maarufu kama mashetani wekundu ametoa orodha ya makipa watakao jiunga kuziba nafasi ya De gea
Share:

LUIS VAN GAAL "DE GEA HAONDOKI MANCHESTER UNITED"

Wakati Meneja wa Manchester United Louis van Gaal akiwa na matumaini Kipa wake David De Gea atabakia huku akiwindwa na Real Madrid, Meneja wa Arsenal Arsene Wenger yuko mbioni kusaka uwiano wa Kikosi chake.
Huko Old Trafford, huku kukiwa na uvumi mzito wa Kipa Nambari Wani David De Gea, mwenye Miaka 21, kuhamia Real Madrid baada ya kusita kusaini Mkataba mpya ulioboreshwa aliopewa na Man United, Meneja Van Gaal amesema: "Bado naamini David De Gea atabaki!"
Licha ya kuumia na kutolewa nje ya Uwanja wakati Man United inatoka Sare 1-1 na Arsenal kwenye Mechi ya Ligi Jumapili iliyopita, Kipa huyo huenda akaanza Mechi yao ya mwisho ya Ligi watakayocheza Ugenini huko KC Stadium dhidi ya Hull City hapo Jumapili.
Kwa Man United Mechi hii ni ya kukamilisha Ratiba tu kwani washaikamata Nafasi ya 4 kwenye Ligi Kuu England lakini kwa Hull City ni lazima washinde ili kuweka hai matumaini yao kubaki Ligi Kuu England.
Baada ya kutolewa kwa De Gea kwenye Mechi hiyo na Arsenal, nafasi yake ilichukuliwa na Kipa wa zamani wa Barcelona na Spain, Victor Valdes, mwenye Miaka 33, ambae alisainiwa Januari Mwaka huu.
Share:

SOMA HAPA RATIBA YA MICHEZO YA MWISHO LIGI KUU UINGEREZA ITAKAYOPIGWA WEEKEND HII


LIGI KUU ENGLAND inafunga Msimu wake wa 2014/15 hapo Jumapili kwa Timu zote 20 kuwa dimbani kwa wakati mmoja kuanzia Saa 11 Jioni kucheza Mechi zao 10 za mwisho.
Tayari Bingwa ameshapatika, ambae ni Chelsea, na nyingine 3 zinazofuatia zitakazocheza UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu ujao zimeshapatikana na hizo ni Man City, Arsenal na Man United.
Pia, Timu 2 kati ya 3 ambazo zitashuka Daraja kucheza Ligi ya Championship Msimu ujao zimepatikana na hizo ni Burnley na QPR na Timu ya 3 kuungana nao itapatikana hiyo Jumapili na ni moja kati ya Newcastle au Hull City.
Hull, ambao wako Nafasi ya 3 toka mkiani wako Pointi 2 nyuma ya Newcastle lakini Hull wana tofauti ya Magoli Bora kupita Newcastle.

Kila Timu inahitaji ushindi hiyo Jumapili maana ikiwa Newcastle itatoka Sare na West Ham watakapocheza Uwanjani Saint James Park, Nyumbani kwa Newcastle, na Hull City, ambao wako Nyumbani KC Stadium, wakiifunga Man United, licha ya sasa kufungana Pointi, basi Hull watapona na Newcastle kushushwa.
Timu zote hizo, Hull na Newcastle, zinacheza na Wapinzani ambao hawana cha maana kwenye Mechi zao mbali ya kukamilisha Ratiba tu.
Lakini Steve Bruce, Meneja wa Hull ambae ni Mchezaji wa zamani wa Man United, anajua fika nini ugumu wa kuifunga Man United maana katika Mechi 21 alizocheza dhidi ya Man United katika Miaka 17 ya kazi yake ya Umeneja hajawahi kuifunga Man United hata mara moja.
Share:

"MOURIHNO WA BONGO" JULIO KUKUTANA NA COAST LEO HII KUJULIKANA ATABAKI MWADUI AU KWA WAGOSI


KOCHA aliyeipandisha daraja Mwadui fc na kwenda kuinusuru Coastal Union kushuka daraja msimu wa 2014/2015 wa ligi kuu soka Tanzania bara, Jamhuri Kiwhelo ‘Julio’ amekiri kuwa ana asilimia kubwa ya kubaki kwa matajiri wa madini wa Mkoani Shinyanga baada ya kufanya mazungumzo ya maana.
Julio amesema kwa takribani asilimia 99 amemalizana na Mwadui ambako atasaini mkataba wa miaka mitatu, lakini ameitwa na Coastal Union, hivyo anakwenda kuwasikiliza kesho jijini Tanga.

“Juzi nimetoka zangu Mwadui kufanya nao mazungumzo, kuna mambo mengi mazuri tumeongea nao kwa takribani asilimia 99. Coastal nao wameniita, naenda kuwasikiliza ni kitu gani wataniambia, baada ya hapo nitaongea kiundani ni wapi nimesimamia, lakini inavyoonekana nina nafasi kubwa ya kubaki Mwadui”. Julio ameiambia E-fm na kuongeza: “Mimi nitasema kile ambacho nimeongea na Mwadui, kibinadamu sio vizuri wenzio wanakuita, halafu unakataa kwa kujiona kama wewe ndio bora kuliko watu wote. Nakwenda kuongea nao kibinadamu, naenda kuwashukuru kwasababu nimefanya nao kazi salama”.
CREDIT: MPENJA
Share:

SOMA HAPA BARUA YA STAND UNITED INAYOKANUSHA TARIFA ZA USAJILI WA JUMA KASEJA NA SALIM MBONDE

BARUA KUTOKA SHINYANGA
Tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa wakazi wa mkoa wa shinyanga,mikoa yote kanda ya ziwa na mashabiki wetu wote walioko nchi nzima na sehemu mbalimbali duniani kwa kutoa ushirikiano wao wa dhati kwetu katika michezo yetu ya ligi kuu tanzania bara msimu wa mwaka 2014-2015 iliomalizika tarehe 9/05/2015.
Tunasema asanteni sana kwa michango yenu ya hali na mali,kifedha,kimawazo na ushauri pia,na hasa katika kipindi kigumu ambacho tumepitia.
ulikuwa ni msimu wetu wa kwanza kushiriki katika ligi mengi tumejifunza na kuona mazuri na magumu katika ligi hii na soka la tanzania kwa ujumla,tunaahidi kuiandaa timu kwa wakati muafaka na kwa weledi mkubwa lengo likiwa ni kufanya vizuri zaidi katika msimu ujao wa ligi kuu Tanzania Bara.
Tunasisitiza kuwa bado hatujaanza kushughurika na swala la usajili wa mchezaji kwasasa na wala hatujafanya mazungumza na mchezaji yoyotekuhusu kumsajili, tunasubiri ripoti ya mwalimu wetu Mathias Rule kujua anapendekeza tufanye nini katika kuboresha timu yetu.
Tunakanusha vikali Taarifa ambazo zinasambaa hivi sasa kuwa tunafanya au tumefanya  mazungumzo na baadhi ya wachezaji ili kuwasajili  akiwemo Juma Kaseja na Beki wa mtibwa sugar Salim Mbonde hatuna mazungumzo na wachezaji hao na hatutafanya usajili wowote bila kupata ripoti ya mwalimu.
kama ripoti ya mwalimu itaelekeza tufanye usajili tutafanya hivyo na uongozi umejipanga kufanya usajili wenye tija na umakini wa kutosha kwa manufaa ya timu yetu ya Stand United fc.
Imetolewa na Idara ya Habari Stand United Fc.
Isaac Edward
Afisa habari.
Share:

TAIFA STARS KURUDI NYUMBANI VICHWA CHINI BAADA YA KUPIGWA NA LESOTHO 1-0

Jana huko Moruleng Stadium, Rustenburg Nchini Afrika Kusini, Tanzania imefungwa 1-0 na Lesotho katika Mechi yake ya mwisho ya Kundi B la COSAFA CUP na hivyo kuaga rasmi Mashindano haya bila kushinda hata Mechi moja.
Mechi hii kwa Timu zote mbili, zenye Pointi 0, ni ya kukamilisha Ratiba tu baada ya wote kutandikwa kwenye Mechi zao mbili za kwanza na kutupwa nje ya Mashindano haya.
Katika Mechi zao mbili za kwanza, Stars ilichapwa 1-0 na Swaziland na kisha 2-0 na Madagascar.
Bao lililoizamisha Taifa Stars lilifungwa Dakika ya 76 na Jeremea Kamela baada ya Frikiki ya Mabuti Potloane kupiga Posti na kumfikia Kamela.

Share:

Friday, 22 May 2015

NDANDA KUOMBA UDHAMINI KWA BILIONEA ANAYETAKA KUNUNUA ARSENAL

Uongozi wa Ndanda FC unajipanga kukutana na bilionea namba moja barani Afrika, Aliko Dangote kwa ajili ya kumuomba kuwa mmoja wa wadhamini wa juu katika timu hiyo kabla msimu ujao haujaanza.

Dangote, raia wa Nigeria, kwa sasa ana kiwanda cha saruji mkoani Mtwara ambako timu hiyo inatokea, anakadiriwa kuwa na utajiri wa pauni bilioni 10.4 (shilingi trilioni 2.7) na hivi karibuni alitangaza nia ya kuinunua Klabu ya Arsenal ya England.
Mwenyekiti wa Ndanda FC, Hamad Omari alisema licha ya kuwa na udhamini wa Kampuni ya Binslum na Big Tanzania, lakini wanajipanga kumuona tajiri huyo anayemiliki kiwanda cha saruji kwenye mkoa wao.
“Tunafikiria kufanya mikakati ya kuweza kukutana naye ili aweze kuwa mdhamini mkuu kwenye timu yetu ambayo imenusurika kushuka daraja.
“Unajua tangu ligi imemalizika bado hatujakaa kuweza kujadili hayo mambo na kama ataweza kukubali basi litakuwa ni jambo jema kwa sababu fedha zinazotolewa na wadhamini wa ligi hazikidhi mahitaji ya timu kwa msimu wote, sasa lazima njia nyingine zitumike kuhakikisha tunakuwa vizuri zaidi msimu ujao,” alisema Omari.

Share:

ANGALIA HAPA TETESI MBALI MBALI ZA USAJILI HAPA TANZANIA KUBWA NI STAND UNITED KUMSAJILI SALIM MBONDE WA MTIBWA

Uongozi wa Stand United ya Shinyanga umefunguka kuwa unamnyemelea beki wa kati wa Mtibwa Sugar, Salim Mbonde ambaye anadaiwa kufuatiliwa na timu za Simba na Yanga.
Stand ambayo imepanga kujiimarisha zaidi katika ligi msimu ujao baada ya kunusurika kushuka daraja, imeeleza kuwa inahitaji kufanya usajili makini ili kuweza kuleta ushindani msimu ujao.
*******************
Siku chache baada ya Yanga kudaiwa kuwa ina mpango wa kuwatema nyota wake 11 wa kikosi hicho, Kocha Mkuu wa JKT Ruvu, Felix Minziro, ameibuka na kuomba apatiwe wachezaji hao.
Baadhi ya wachezaji ambao Yanga inadaiwa kutaka kuwafungashia virago klabuni hapo ni Jerry Tegete, Hussein Javu, Danny Mrwanda, Nizar Khalfan, Rajabu Zahir, Edward Charles na Hassan Dilunga.
***********************
Kamati ya Usajili ya Simba, imefanya kweli kwa kuwabakiza wachezaji wake wawili, Said Ndemla na Hassan Isihaka.
Isihaka ambaye ni nahodha wa Simba, ilielezwa alikataa kusajili kwa madai nataka dau nono zaidi.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia hans Poppe amesema tayari wamemalizana na wachezaji hao kwa kuwaongezea mikataba ya miaka mitatu kila mmoja.
*********************
Uongozi wa Klabu ya Simba umemtega kiungo wake mshambuliaji, Ramadhan Singano ‘Messi’ kwa kumtaka atafakari kwa mara nyingine kuhusu dau la shilingi milioni 30 alilotajiwa, badala ya shilingi milioni 50 anazotaka.
Singano ambaye alipandishwa kutoka kikosi cha Simba B, inaelezwa kuwa anatembea na mkataba aliopewa kwa kuwa anahitaji kutafakari kabla ya kusaini.
Share:

JOSE MOURIHNO NDIYE KOCHA BORA LIGI KUU UINGEREZA

Mkufunzi wa klabu ya Chelsea Jose Mourinho ametangazwa kuwa mkufunzi bora katika ligi ya Uingereza kwa mara ya tatu.
Akihudumia kipindi chake cha pili katika kilabu hiyo rais huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 52 aliiongoza Chelsea kubeba taji lao la kwanza la ligi ya Uingereza katika kipindi cha miaka mitano pamoja na kombe la Ligi.
Share:

DAVID LUIZ :NINA DEMU NA NIMEWAHI KUFANYA MAPENZI

Mlinzi wa klabu ya Paris St-Germain David Luiz amevishtumu vyombo vya habari kwa kukosa heshima baada ya kukanusha madai kwamba yeye hajawahi kushiriki katika tendo la ngono.

Ripoti hizo zilianza kusambaa baada ya mchezaji huyo wa zamani wa Chelsea mwenye umri wa miaka 28 kusema katika instagram kwamba yeye na mpenziwe ''wako tayari kungojea''.
Aliiambia BBC focus kwamba.''Dini yangu,ubaatizaji wangu,nafurahia.
Watu wanasema maneno kila mahala kuhusu iwepo mimi sijawahi fanya tendo la ngono.''Ukweli ni kwamba mimi nishawahi kushiriki katika tendo hilo''.
Share:

ANGALIA NKURUZINZA ANAVYOPIGA SOKA WAKATI NCHI YAKE IKIENDELEA NA VURUGU ZA KISIASA

Pamoja na hali ya vurugu inayoendelea nchini Burundi, Rais wa nchi hiyo, Pierre Nkurunziza ameamua kujipoza kwa kucheza soka.
Nkurunziza aliyeokoka baada ya jaribio la kutaka kumpindua, amefanikiwa kurejea madarakani.
Sasa anataka kuwania nafasi ya urais kwa muhula wanne na wananchi wamekuwa wakipinga hilo.




Share:

LUIS FIGO NA MICHAEL VAN WAJITOA KUWANIA URAIS FIFA SOMA HAPA SABABU

Wagombea wawili kati ya wanne waliojitokeza kuwania nafasi ya urais wa shirikisho la vyama vya soka Duniani FIFA wamejitoka katika kinyang'ang'anyiro hicho.

Nyota wa zamani wa soka huko Ureno , Luis Figo ambaye ni mmoja wa waliojitoa kuwania nafasi hiyo,amelalamikia mfumo wa uendeshaji wa uchaguzi huo na kuiita kuwa ni wakinafiki.

Amesisitiza kuwa kwa mtazamo wake anaona kuwa taratibu zilizowekwa zililenga kumnufaisha mgombea mmoja tu na si kuelta usawa wa wote waliojitokeza kuwania nafasi hiyo,ambapo inaonekana kuwa ni mpango uliowekwa kumpatia nafasi ya ushindi Rais wa sasa Sepp Blatter ambaye anawania nafasi hiyo kwa kipindi cha tano.

Hata hivyo Rais wa chama cha soka huko Uholanzi , Michael van Praag , akijitoa. Huku wapinzani waliosalia ni Bw Blatter ambaye ni Jordan Prince Ali Al Hussein ambaye ni mwanachama wa kamati ya utendaji ya FIFA.

Mgombea mwingine aliyejitoa pia ni Rais wa chama cha soka cha Uholanzi Michael van Praag na hivyo kuwaacha Blatter na mtu anayedaiwa kuwa mpinzani wake wa karibu Prince Ali Al Hussein ambaye ni mjumbe wa kamati ya utendaji ya FIFA
Share:

KLABU YA SUNDERLAND YA UINGEREZA YAENDESHA MAFUNZO YA SOKA HUKO MARA

Klabu ya Ligi Kuu England Sunderland hivi karibuni imetembelea Tanzania ikiongozwa na Mkuu wao wa Kuendeleza Soka Kimataifa, Graham Robinson, ambae alizuru Migodi Miwili inayomilikiwa na Acacia Mining ili kutoa Mafunzo ya Soka kwa Jamii zinazoishi jirani na Migodi hiyo.
Acacia Mining plc, ndiyo inayomiliki Migodi ya Dhahabu ya Bulyanhulu, Buzwagi na North Mara.
Ziara hiyo ya Graham ni Mradi wa pamoja wa Klabu ya Sunderland na Acacia Mining ili kutoa Mafunzo ya Soka na Ukocha kwa Timu za Migodi hiyo na Makocha wao.
Mafunzo hayo yalifanyika Bulyanhulu Mine School yakijumuisha Makocha wa Timu ya Acacia pamoja na Makocha kutoka Vijiji jirani.
SAFC - Acacia
Akiongelea kuhusu Mafunzo hayo, Graham alisema: "Tulitoa mafunzo ya vitendo kadhaa na Makocha walishiriki kikamilifu na kuuliza maswali mengi."
"Soka ya Jamii ndio chanzo cha Wachezaji wengi na kupitia Washirika wetu Barani Afrika tuna Miradi ya muda mrefu na tunasifika kwa kuwekeza katika Programu za Elimu katika Jamii."  

Share:

TANZANIA KUTUPA KARATA YAKE YA MWISHO LEO DHIDI YA VIBONDE WENZAO LESOTHO JE KUENDELEZA KUPOTEZA AU?

Leo huko Moruleng Stadium, Rustenburg Nchini Afrika Kusini, Tanzania inacheza Mechi yake ya mwisho ya Kundi B la COSAFA CUP dhidi ya Lesotho.
Mechi hii kwa Timu zote mbili, zenye Pointi 0, ni ya kukamilisha Ratiba tu baada ya wote kutandikwa kwenye Mechi zao mbili za kwanza na kutupwa nje ya Mashindano haya.

Kwa Mashabiki wa Tanzania, wengi wakikasirishwa na kufungwa na Timu za chini yao kwa mbali kwenye Listi ya FIFA UBORA DUNIANI, Leo ndio itajulikana wazi kwamba 'Taifa Stars bado Kichwa cha Mwenda Wazimu!'
Mechi nyingine ya Kundi B hii Leo ni kati ya Madagascar na Swaziland na mmoja kati yao atatinga Robo Fainali kuikwaa Ghana.
Kwenye Kundi A, Namibia iliibamiza Zimbabwe Bao 4-1 na kutinga Robo Fainali kuwavaa Mabingwa Watetezi wa Kombe hili Zambia.
Share:

Thursday, 21 May 2015

KOCHA MPYA WA SIMBA PIET DE MOL ATUA LEO JIJINI DAR KUFANYA MAZUNGUMZO KUIFUNDISHA TIMU HIYO

KOCHA Mbelgiji Piet de Mol aliyekuwa anawania kurithi mikoba ya Goran, amewasili leo Dar es Salaam na kwenda kukaa meza moja na Mratibu wa Mtibwa Sugar, Jamal Bayser.
Mtibwa walimtumia usafiri de Mol Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam, ambao ulimpeleka kwenye ofisi za Mratibu wake, Jamal Bayser, barabara ya Nyerere.
Mara moja Mtibwa wakafanya mazungumzo na kocha huyo na taarifa za awali zinasema wamemalizana, kilichobaki ni klabu huyo bingwa ya zamani nchini yenye maskani yake, Turiani, Morogoro kutangaza ndoa hiyo na Mbelgiji huyo.

Mwalimu huyo mwenye umri wa miaka 60 ambaye ana uzoefu mkubwa wa kufundisha soka Afrika, Asia na Ulaya anaweza kuwa bosi wa kocha Mkuu wa sasa Mtibwa, Mecky Mexime.

Mwaka jana, Piet de Mol alikuwa nchini Ghana akifanya kazi kama Mkurugenzi wa Ufundi wa akademi mjini Kumasi
Mbali na Ghana ambako alifanya kazi na Asante Kotoko, De Mol amefundisha timu pia kwao Ubelgiji, Dubai, Qatar na China. Alikuwa kocha Msaidizi wa AA Gent kuanzia mwaka 1997 hadi 2001.
Ilibaki kidogo Mbelgiji huyo arithi mikoba ya Mserbia, Goran Kopunovic klabu ya Simba SC ambayo awali ilishindwa kufikia makubaliano ya Mkataba mpya na kocha huyo aliyetaka kiwango cha fedha.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe aliiambia BIN ZUBEIRY wiki iliyopita kwamba Kopunovic alitaka dola za Kimarekani 50,000 (sawa na Sh. Milioni 100) kama dau la kusaini Mkataba na dola 8,000 (Sh. Milioni 16).
Lakini sasa Kopunovic, aliyeiongoza Simba SC katika mechi 24 tangu aanze kazi Januari mwaka huu kati ya hizo, timu imeshinda mechi 18, sare mbili na kufungwa nne, amekubali kurudi kazini Msimbazi.

SOURCE: BIN ZUBERY
Share:

ARSENAL YAKABWA NA SUNDERLAND WAKITOKA SARE 0-0 SASA SUNDERLAND KUJINUSURU NA KUSHUKA DARAJA

Jana Usiku Sunderland, wakiwa Ugenini Uwanjani Emirates katika Mechi ya Kiporo na Arsenal, walimudu kupata Sare waliyokuwa wakiihataji ili kujinusuru balaa la kushuka Daraja kutoka Ligi Kuu England baada ya kutoka 0-0.
Tayari Timu mbili, QPR na Burnley, zishashuka Daraja na bado Timu moja inatakiwa kuungana nao na sasa moja ya hizo itakuwa Hull City au Newcastle.
Shujaa mkubwa wa Sunderland hapo Jana ni Kipa wao Costel Pantilimon alieokoa michomo kadhaa toka kwa Mafowadi wa Arsenal lakini hata Sunderland wangeweza kushinda Mechi hii na hasa pale Fowadi wao Steven Fletcher alipopoteza nafasi.
Furaha kubwa ilikuwa kwa Meneja wa Sunderland, Dick Advocaat, ambae aliletwa zikibaki Mechi 8 kuiokoa Timu hiyo kutoshuka Daraja baada ya kutimuliwa Gus Poyet.

Share:

ANGALIA TETESI MBALIMBALI ZA USAJILI ULAYA STORI KUBWA RAHEEM STERLING KUTUA MANCHESTER CITY AU BAYERN

RAHEEM STERLING AWANIWA NA MAN CITY,ARSENAL NA BAYERN MUNICH
Huku kukiwa na ripoti kuwa Mchezaji Bora Kijana wa Liverpool kwa Msimu huu, Raheem Sterling, akiwa njiani kuiambia rasmi Klabu yake anataka kuhama na Chelsea, Manchester City, Arsenal na Bayern Munich zikimlilia, Mahasimu wakubwa wa Liverpool, Manchester United, nao wamejitumbukiza kumuwania.
Licha ya kuwepo nafasi duni kwa Liverpool kukubali kuwauzia wapinzani wao wakubwa Man United Staa wao, imeripotiwa kuwa Mawakala toka Old Trafford wamepiga hodi kuulizia kuhusu uwezekano wa kumnunua Sterling.
Inatarajiwa Ijumaa Jioni, Raheem Sterling na Mwakilishi wake, Aidy Ward, watakutana na Meneja wa Liverpool Brendan Rodgers pamoja na Mtendaji Mkuu wa Klabu hiyo, Ian Ayre, na hapo ndipo rasmi Sterling atatamka kutaka kuihama Liverpool Msimu huu.
Ripoti pia zimedai kuwa Liverpool imeijulisha Man United kuwa Sterling si biashara kwao kwa Dau lolote. 
Lakini Wachambuzi wanahisi mlengwa mkuu wa Sterling ni Man City ambao wako tayari kumlipa Winga huyo Chipukizi wa England mwenye Miaka 21 Mshahara wa Pauni 150,000 kwa Wiki badala ya Pauni 100,000 aliyopewa Ofa mpya kwenye Mkataba mpya na Liverpool ambao ameukataa.
*****************************
XAVI KUONDOKA BARCELONA
Kiungo wa Barcelona Xavi yupo tayari kutangaza kuwa anaondoka Barcelona kwenda kujiunga klabu ya nchini Qatari Al Sadd kwa mkataba wa miaka mitatu, anasema wakala wake.
Xavi, 35, amekuwa na miamba hiyo ya La Liga kwa miaka 17, akishinda mataji manane ya La Liga, mataji matatu ya Champions League na mataji mengine kadhaa.
Mchezo wake wa mwisho wa ligi kukipiga kwa mabingwa wapya wa La Liga utakuwa dhidi ya Deportivo La Coruna Jumamosi ijayo.
Barcelona bado ina nafasi ya kutwaa Champions League na Copa del Rey.
Kwa mujibu wa wakala wake, Ivan Corretja, Xavi anaweza pia kuwa balozi wa Kombe la Dunia mwaka 2022 ambalo litafanyika nchini humo kabla ya kuanza harakati zake za kuwa kocha.
Xavi ameichezea timu ya taifa ya Uhispania mara 133 - ikiwa ni rekodi - na alikuwa sehemu muhimu ya ushindi wa Kombe la Dunia mwaka 2010 na ubingwa wa Ulaya mwaka 2008 na 2012.
******************************
Fowadi wa Real Madrid Gareth Bale, 25, anataka kubaki kwenye klabu hiyo yaLa Liga, akifikisha mwisho matumaini ya Manchester United kumtumia kama dili la kumnasa kupitia mlinda mlango David De Gea, 24. (Mirror)
Bale aliambiwa kubaki klabu hapo ikiwa ni mipango ya muda mrefu ya Real kwenye mkutano na wakurugenzi wa klabu. (Sun)
****************************
Meneja wa Chelsea Jose Mourinho anafikiria kutoa ofa kwa mshambuliaji wa Aston Villa kutoka Ubelgiji Christian Benteke, 24, ambaye ana thamani ya paundi 30m. (Daily Mirror)
Mlinzi wa kimataifa wa Ujerumani na klabu ya Borussia Dortmund Mats Hummels, 26 - ambaye anawindwa kwa muda mrefu na klabu ya Manchester United - ameamua kukataa kuhamia England. (Bild - in German)
*************************
Manchester City na Chelsea zinamuwania kiungo wa Barcelona Alex Song, 27. Song amekuwa kwa mkopo kwenye klabu ya West Ham. (Mail)
************************
City pia wanamuwinda mshambuliaji wa West Brom Saido Berahino, 21. (Daily Star)
Wakati huo huo, Yaya Toure, 32, anaonekana na kila dalili za kuondoka Etihad, ambapo Inter Milan wanakaribia kumnasa kiungo huyo wa kimataifa wa Ivory Coast. (The Times)
****************************
Liverpool itatangaza kuwa winga Jordon Ibe, 19, amesaini mkataba mpya wa miaka mitano wenye thamani ya paundi 35,000 kwa wiki. (Sun)

Share:

JUVENTUS WATWAA COPPA ITALIA SASA KULIWINDA TAJI LA UEFA

Alessandro Matri amekuwa Shujaa asietarajiwa baada ya kutoka Benchi na kufunga Bao la ushindi katika Dakika za Nyongeza 30 na kuipa Juventus ushindi wa Bao 2-1 dhidi ya Lazio katika Fainali ya Coppa Italia ambayo imeweka hai ndoto yao ya kutwaa Trebo Msimu huu.
Matri, ambae amekuwa akihama Klabu katika Madirisha ya Uhamisho manne yaliyopita na kutua Juve Mwezi Januari akipigwa Benchi tu, alifunga Bao hilo la ushindi katika Dakika ya 7 ya Dakika za Nyongeza 30 baada ya Sare ya 1-1 katika Dakika 90.
Hii ni mara ya 10 kwa Juve kutwaa Coppa Italia, ambayo ni Rekodi, lakini mara ya mwisho kubeba Kombe hili ni Mwaka 1995.
Baada ya kutwaa Ubingwa wa Serie A mara 4 mfululizo na sasa kubeba Coppa Italia, Juve wapo njiani kutwaa Trebo, yaani Mataji Matatu, kwa vile pia Juni 6 watacheza Fainali ya UEFA 
Share:

TAIFA STARS YATUPWA NJE MICHUANO YA COSAFA KESHO KUREJEA NYUMBANI

Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) jana imepoteza mchezo wa pili mfululizo katika michuano ya kombe la Cosafa, baada ya kufungwa mabao 2 - 0 na Madagascar, mchezo uliofanyika katika uwanja wa Royal Bafokeng jijini Rustenburg.
Kwa Taifa Stars kupoteza mchezo huo, moja kwa moja inakua imeaga michuano katika hatua ya makundi, kutokana na kubakisha mchezo mmoja tu wa kukamilisha ratiba dhidi ya Lesotho utakaochezwa kesho ijumaa katika uwanja wa Moruleng.
Katika mchezo huo wa jana, Taifa Stars ilishindwa kuonyesha makali yake mbele ya timu ya Madagascar na kupelekea kufungwa mabao 2 katika dakika 45 za kipindi cha kwanza.
Sehemu ya ushambuliaji ya Taifa Stars haikua na madhara yoyote langoni mwa Madagascar, huku sehemu ya ulinzi iLijikuta na wakati mgumu muda wote kuzuia hatara za washambuliaji wa Madagascar.
Mara baada ya mchezo huo, kocha wa Stars Mart Noij alisema amesikitishwa na matokeo hayo, kwamba hakutegemea kupoteza mchezo dhidi ya Madagascar.
“Timu yangu haikucheza vizuri, haikuweza kutengeneza nafasi nyingi za kufunga , huku wapinzani awetu wakitumia nafasi mbili walizozipata kupata mabao mawili katia mchezo huo” alisema Nooij.
Mpaka sasa kundi B la linaongozwa na Madagscar yenye ponti 6 sawa na Swaziland yenye pointi 6 pia zikiwa na tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa, na mchezo wa mwisho utakaowakutanisha kesho ndio utakaoamua nani atatinga hatua ya robo fainali.
Kufuatia Taifa Stars kupoteza michezo yote miwili, inaungana na Lesotho kutoka kundi B kuaga michuano hiyo, huku kundi A timu za Mauritius na Shelisheli zikiwa zimeshaaga michuano hiyo pia.
Stars inatarajiwa kurejea nyumbani Tanzania kesho ij
umaa usiku mara baada ya mchezo wake wa mwisho dhidi ya Lesotho utakochezwa kesho jioni.
Share:

Tuesday, 19 May 2015

MABNGWA WA UINGEREZA NA CAPITAL ONE WALA KIPIGO CHA GOLI 3-0 DHIDI YA WEST BROMWICH ALBION

Mabingwa wapya wa Ligi Kuu England Chelsea wametandikwa Bao 3-0 huko The Hawthorns na West Bromwich Albion katika Mechi ya Ligi Kuu England.
Mechi hii, ambayo ni kiporo kwa Timu hizi, ni ya kukamilisha ratiba tu hasa kwa Chelsea ambao walikuwa tayari washatwaa Ubingwa wa England wakiwa na Mechi kadhaa mkononi.

Hata hivyo, Chelsea walishusha Kikosi imara lakini Saido Berahino aliwapa WBA Bao lao kwanza Dakika ya 9 kufuatia pasi safi kati ya Chris Brunt na Joleon Lescott na yeye kupasiwa mwisho na kuachia Shuti la juu toka Mita 20.
Dakika ya 29, Chelsea walibaki Mtu 10 baada ya Kiungo wao Cesc Fabregas kupewa Kadi Nyekundu na Refa Mike Jones kufuatia kumpiga kwa makusudi na Mpira Chris Brunt wakati wa mzozo kati ya Olsson wa WBA na Diego Costa ambao Refa huyo alikuwa akiusuluhisha.
Hadi Mapumziko, WBA 1 Chelsea 0.
Dakika moja tu tangu Kipindi cha Pili kuanza, Nahodha wa Chelsea John Terry alimwangusha Saido Berahino ndani ya Boksi na WBA kupewa Penati na Berahino kuipiga na kufunga Bao lake la pili na kuifanya WBA iwe mbele 2-0 dhidi ya Mabingwa wa England Chelsea.
Chris Brunt aliipa WBA Bao la 3 katika Dakika ya 60 alipoanzisha mwenyewe Kona fupi na kumpasia James Morrison aliemrudishia Brunt ambae Shuti lake lilimhadaa Kipa Courtois na kutinga.
Share:

Monday, 18 May 2015

MICHUANO YA COSAFA TIMU YA TAIFA YA TANZANIA YACHEZEA KICHAPO CHA GOLI 1-0 DHIDI YA WASWAZI

Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, imeanza Mechi zake za Kundi B la COSAFA CUP huko Royal Bafokeng Sports Palace, Phokeng, Rustenburg, Nchini South Africa kwa kufungwa Bao 1-0 na Swaziland. 
COSAFA CUP hushindaniwa na Nchi za Afrika ya Kusini na Mwaka huu Tanzania na Ghana zimealikwa kushiriki. 
Licha ya kupata nafasi kadhaa, Taifa Stars walijikuta wakifungwa kwenye Dakika ya 44 kwa Shuti la Sifiso Mabila kumshinda Kipa Munish.
Hadi Mapumziko Taifa Stars 0 Swaziland 1.
Bao hilo moja lilidumu hadi mwisho wa mchezo na kuiacha Taifa Stars ikishika Nafasi ya 3 katika Kundi B ambalo Madagascar, walioifunga Lesotho 2-1 mapema Leo, wakiongoza na kufuatiwa na Swaziland huku Lesotho wakiwa mkiani.
Mechi inayofuata kwa Taifa Stars ni hapo Jumatano Mei 20 dhidi ya Madagascar.
VIKOSI:
Tanzania: Deogratias Munish, Agrey Ambros, Salim Mbonde, Oscar Fanuel, Erasto Nyoni, Said Juma, Saimon Msuva, Shomari Kapombe, Mwinyi Kazimoto, Mrisho Ngasa, John Bocco.
Swaziland: Mphikeleli Dlamini, Sifiso Mabila, Siyabonga Mdluli, Sanele Mkhweli, Zweli Nxumalo, Mthumzi Mkhontfo, Siboniso Malambe, Machawe Dlamini, Njabulo Ndlovu, Tony Tsabedze, Xolani Sibandze.
Share:
Powered by Blogger.

IDADI YA WANAOTEMBELEA BLOG HII

Blog Archive

Recent Posts

Fashion

3/Fashion/big-col-right

Recent Posts

Header Ads

Followers

Powered By Blogger

Tags

Maoni

3/recent-comments

WASILIANA NASI

Popular Posts

Labels

Blog Archive

Blogger templates