Pages

Thursday, 25 June 2015

COPA AMERICA CHILE WATINGA NUSU FAINALI

Wakicheza kwao Estadio Nacional de Chile, Santiago, Chile wameifunga Mtu 9 Uruguay Bao 1-0 na kutinga Nusu Fainali ya Kombe la Mataifa ya Marekani ya Kusini, COPA AMERICA.
Bao hilo la Chile lilifungwa na Mauricio Isla katika Dakika ya 81 wakati Uruguay, Mabingwa Watetezi, wakicheza Mtu 10 baada ya Edinson Cavani kutolewa kwa Kadi Nyekundu katika Dakika ya 63 kufuatia Kadi ya Njano ya Pili.

Cavani alipewa Kadi ya Njano ya kwanza katika Dakika ya 29.
Katika Dakika ya 88 Uruguayl ilibaki Mtu 9 baada Jorge Fucile kupewa Kadi Nyekundu baada kujizolea Kadi za Njano mbili.
Kwenye Nusu Fainali, Chile watacheza na Mshindi kati ya Bolivia na Peru wanaocheza Usiku huu.
Share:

BAADA YA JANA GONZALO JARA KUMFANYIA VIBAYA CAVAN JARA AFUNGIWA MECHI ZILIZOBAKI COPA AMERICA

jara


Picha zimeoonyesha Gonzalo Jara alimfanyia kitendo kibaya Cavari wakiwa uwanjani kwenye mechi ya robo fainali. Lakini baada ya kitendo hicho Cavari alimfanya madhabi Jara na akapewa kadi nyekundu na kutolewa nje ya uwanja.
Baada ya kitendo kile kupitiwa hivi sasa imetoka adhabu kwenda kwa Gonzalo kwamba amefungiwa kucheza michezo iliyobakia ya Copa America. Nchi yake ya Chile itamkosa kwenye mechi ya nusu fainali au fainali kama wakiingia
Share:

USAJILI TANZANIA : KIONGERA AREJEA SIMBA HALI SI NZURI BAADA YA VIPIMO APEWA MAPUMZIKO YA MWEZI MMOJA


MSHAMBULIAJI Mkenya wa Simba SC, Paul Mungai Kiongera atahitaji mwezi wa mapumziko kabla ya kuanza tena kuichezea timu hiyo.
Tovuti ya Simba SC imeandika leo kwamba, Kiongera aliwasili jana nchini na kufanyiwa vipimo, ambavyo vimegundua kwamba anahitaji mwezi mmoja wa zaidi wa mapumziko.
“Vipimo hivyo vya afya vilifanyika leo saa tano asubuhi na baada ya vipimo Daktari wa timu alishauri Kiongera kupewa mapumziko ya mwezi mmoja kabla ya kujiunga na timu rasmi,”imeandika tovuti rasmi ya Simba SC.

Kiongera alisajiliwa Simba SC msimu uliopita kutoka KCB ya kwao, Kenya lakini baada ya wiki tatu akatonesha goti lake na kwenda kufanyiwa upasuaji India.
Kwa kuwa usajili ulikuwa haujafungwa, Kiongera aliondolewa kwenye orodha ya wachezaji wa Simba SC wa msimu uliopita ili nafasi yake asajiliwe mchezaji mwingine.
Hata hivyo, Kiongera baada ya kupata nafuu alisajiliwa na KCB ambayo aliichezea katika Ligi Kuu ya Kenya.
Baada ya kufunga mabao kadhaa ya kusisimua katika Ligi Kuu ya Kenya, Simba SC ilijiridhisha mshambuliaji huyo amepona na ikaamua kumrejesha kikosini.

Share:

STARS YA WATOTO KUELEKEA MBEYA KESHO TAYARI KWA MECHI DHIDI YA KOMBAINI YA MBEYA

Kikosi cha timu ya Taifa ya Vijana wenye umri chini ya miaka 15 (U-15) kesho ijumaa kinatarajia kusafiri kuelekea jijini Mbeya kwa ajili ya mchezo wa kirafiki na timu kombani ya mbeya U15.
U15 ambayo inanolewa na kocha Bakari Shime, itaondoka na kikosi cha wachezaji wa thelathini (30) ambapo wanatarajiwa kucheza michezo miwili ya kirafiki na timu ya kombani ya mkoa wa Mbeya ya vijana wenye umri chini ya miaka 15.
Timu itacheza michezo ya kirafiki siku ya jumapili na jumatatu ambapo kocha Shime atatumia nafasi hiyo kutambua uwezo wa wachezaji wake na kuongeza wachezaji wengine watakaonekana kutoka katika kombani ya mkoa wa Mbeya.

Mwezi ujao kikosi cha U-15 kitaelekea kisiwani Zanzibar kucheza michezo ya kirafiki na timu za kombaini ya Zanzibar kisha baadae kuendelea na ziara ya kucheza michezo ya kirafiki katika mikoa ya Iringa, Morogoro, Tanga, Arusha, Mwanza na Dodoma.
Lengo la TFF ni kuhakikisha Tanzania inakua na kikosi bora cha timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 kitachoshiriki kuwania kufuzu kwa fainali za vijana Afrika wenye umri chini ya miaka 17 mwaka 2017 nchini Madagascar
Share:

TANZANITE QUEENS TIMU YA TAIFA YA WANAWAKE U-20 INAINGIA KAMBINI CHAMAZI

Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu ya Wanawake wenye umri chini ya miaka 20 (U-20) Tanzanite Stars, imeingia kambini jana jioni Mbande jijini Dar es salaam na itakua ikifanya mazoezi katika uwanja wa Azam Complex.
Kikosi cha wacheaji 22 chini ya Kocha Mkuu Rogasian Kaijage kinafanya mazoezi asubuhi na jioni katika uwnaja wa Azam uliopo Chamazi kujiandaa na mchezo dhidi ya U-20 ya Zambia utakaofanyika kati ya tarehe 10, 11 na 12 July jijini Dar es salaam.
Mchezo huo dhidi ya Zambia ni wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Wanawake za Dunia wenye umri chini ya miaka ya 20, zitakazofanyika nchini Papua New Guinea mwaka 2016.

Wachezaji waliopo kambini ni, Najiati Abbasi, Zuwena Aziz, Shelder Boniface, Stumai Abdallah, Donisia Daniel, Tatu Iddy (Evergreen Queens), Niwael Khalfani, Maimuna Hamis (Mburahati Queens), Anastazia Anthony, Amisa Athumani, Amina Ramadhani, Neem Paulo (JKT Queens).
Wengine ni Asha Shaban, Rebeka Daniel, Brandina Wincelaus (Tanga), Happines Hezroni, Jane Cloudy (JKT Queens), Wema Richard, Gerwa Lugomba, Sadda Ramadhani (Uzuri Queens), Anna Hebron (Evergreen Queens) na Shehati Mohamed (Mburahati Queens)
Aidha wachezaji Monica Henry, Tumaini Michael (Uzuri Queens), Diana Msewa (Mbeya), na Vailet Nicolaus (Evergreen) bado hawajaripoti kambini wanaombwa kuripoti na kuungana na wenzao katika maandalizi ya mchezo huo dhidi ya Zambia.
Share:

TRA YAINGIA KWENYE SOKA SASA TIMU ZAAMURIWA KUWALIPIA KODI MAKOCHA NA WACHEZAJI WAKE

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeviagiza vilabu vinavyoshiriki Ligi kuu ya nchini (mpira wa kulipwa) Tanzania, kuhakikisha kuwa wanalipa kodi kutokana na kuajiri makocha na wachezaji kutoka ndani na nje ya nchi.
Kamshina wa TRA ameliagiza Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) kupitia kwa katibu mkuu wake kuwa, vilabu vyote vya mpira wa miguu nchini vinavyoajiri walimu, wachezaji kutoka ndani na nje ya nchi wahakikishe wanaweka kipengele cha kodi katika mikataba wanayoingia kuwaajiri.

Vilbu vya vinapaswa kuwasilisha mikataba yote ya ajira ya wachezaji na walimu wao ili kukokotoa kodi stahiki kwa kila mmoja wao na mikataba yao kugongwa muhuri na stempu.
Kwa mujibu wa sheria za Kodi ya Mapato ya mwaka 2004, kufungu namba 7, kila mtu anayepata mapato yatokanayo na ajira katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anawajibika kulipa kodi ya mapato kulingana na kipato chake.
Aidha kwa mujibu wa Sheria ya Ushuru wa stempu ya mwaka 1973, kifungu namba 5 kikisomwa pamoja na jedwali la sheria hii, kila mkataba unatakiwa kugongwa muhuri na stempu na ofisa wa stempu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania.
Kwa kuwa TFF ndio mlezi na msimamizi mkuu wa vilabu vya Mpira wa Miguu hapana nchini na hasa Ligi Kuu, tunaviomba vilabu vyote kuhakikisha vinawasilisha mikataba ya walimu na wachezaji yao ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa ajili ya kugongwa mihuri na stempu.
Share:

Wednesday, 24 June 2015

SOMA HABARI ZA USAJILI TANZANIA LEO JUMATANO KUBWA NI RUVU SHOOTING WAGOMA KUMSAJILI BEKI WAO GEORGE MICHAEL

Pamoja na kikosi cha Ruvu Shooting kushuka daraja, uongozi wa Maafande hao umefunguka kuwa haupo tayari kumpeleka beki wake, George Michael ‘Beki Katili’ katika timu yoyote hata kama ya jeshi kwa sababu bado wana mkataba naye.
Awali iliripotiwa kuwa JKT Ruvu ilipeleka maombi kwa ajili ya kumuomba beki huyo kuongeza nguvu kwenye kikosi chao msimu ujao.
Ofisa habari wa timu hiyo, Masau Bwire alifunguka kuwa beki huyo watashuka naye na hakuna timu ambayo inaruhusiwa kumchukua.
******************
iungo wa Klabu ya Simba Jonas Mkude anatarajiwa kwenda Afrika Kusini Alhamisi Juni 26 mwaka huu kwa majaribio ya wiki mbili katika Klabu ya Bidvest Wits.
Akiongea na tovuti ya Simba, Mkude alisema fursa hii ni adimu na anaamini akifanikiwa ataiwakilisha vyema Simba na Tanzania kwa ujumla. 

Akizungumzia pengo litakaloachwa ikiwa atafanikiwa majaribio alisema “pengo langu linaweza kuzibwa kwani Simba ina wachezaji nyota wanaojituma na wenye uwezo”
***********************
Wakala wa mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania Mbwana Samatta, Jamal Kisongo amesema hatma ya mshambuliaji huyo kucheza soka la kulipwa Ulaya sasa itasubiri mwakani kutokana na rais na mmiliki wa klabu yake yake TP Mazembe Moise Katumbi kuonesha bado anahitaji huduma yamchezaji huyo hususan katika michuano ya vilabu bingwa barani Afrika.***********************
Kocha Mkuu wa Yanga Mholanzi, Hans Pluijm ametamka kuwa wachezaji wawili wa Ghana wakati wowote wanatarajiwa kutua nchini kujiunga na kikosi hicho kwenye msimu ujao wa Ligi Kuu Bara na Ligi ya Mabingwa Afrika, mwakani.
Kauli hiyo, ameitoa ikiwa ni siku chache tangu Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitia kamati yao ya utendaji kuruhusu klabu za ligi kuu kusajili wachezaji saba wa kimataifa.
Share:

SIMBA KUMKOSA MAVUGO KISA DENI LA TAMBWE KWA VITAL O

Pamoja na kufanya jitihada za kumnasa mshambuliaji Laudit Mavugo, Simba bado inadaiwa na Vital’O ya Burundi na imekiri.
Vital’O inaidai Simba dola 5,000 (zaidi ya Sh milioni 10) ikiwa ni sehemu ya fungu la usajili wa Amissi Tambwe.
Tayari Tambwe yuko Yanga baada ya Simba kumtema, lakini bado hawajalipwa fedha hizo.

Taarifa za awali zilieleza kuwa deni hilo limevuruga hata usajili wa Mavugo kwa Vital’O kutaka kulipwa kwanza fedha za Tambwe.
Lakini uongozi wa Simba kupitia mjumbe wake wa kamati ya utendaji, Collins Frisch ikatoa ufafanuzi kwamba la hasha.
“Hakika hilo deni lipo na tumelikubali hata kama lilikuwa wakati wa uongozi uliopita, lakini Simba ndiyo hii,” alisema Frisch.
“Lakini tumeelewana vizuri na Vital’O na tuko katika mchakato wa kulipa lakini hilo halijaingiliana na usajili wa Mavugo, si kweli.”
Share:

KOCHA MPYA WA STARS ATAJA KIKOSI KISOME HAPA DIDA, NYONI,KIEMBA WATEMWA


Kocha mpya wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa aliyechukua nafasi ya Mart Nooij ametangaza kikosi chake kipya kwa ajili ya kuivaa Uganda huku akimtema kipa Deogratius Munish ‘Dida’ na nafasi yake amemchagua Ally Mustapha ‘Barthez’.
Wengine ambao Mkwasa amewatema ni Erasto Nyoni, Amri Kiemba na Kelvin Friday kutoka Azam FC pia Oscar Joshua kutoka Yanga, Pia Ibrahim Ajibu kutoka Simba.
Waliorejea ni Kelvin Yondani pia Deus Kaseke huku akimchukua Michael Idan wa Ruvu Shooting.
Pia Samuel Kamuntu wa JKT, Juma Abdul wa Yanga na Mudathir Yahya kutoka Azam wamejumuishwa kwamba wanaweza kuitwa wakati wowote.

KIKOSI KAMILI:
Mwadini Ally-Azam
Ally Mustapha-Yanga
Mudathir Khamis-KMKM
Shomari Kapombe-Azam
Michael Haidan-Ruvu Shooting
Mohammed Hussein-Simba
Mwinyi Hajj-KMKM
Nadir Haroub-Yanga
Kelvin Yondani-Yanga
Aggrey Morris-Azam
Hassan Isihaka-Simba
Jonas Mkude-Simba
Abdi Banda-Simba
Simon Msuva-Yanga
Said Ndemla-Simba
Ramadhan Singano-Simba
Salum Telela-Yanga
Frank Domayo-Azam
Atupele Green-Kagera Sugar
Rashid Mandawa-Mwadui
Ame Ally-Azam
Deus Kaseke-Yanga
Share:

Monday, 22 June 2015

SIMBA IMEMTANGAZA KOCHA MPYA KUTOKA UINGEREZA


Klabu ya Simba imeingia mkataba na Dylan Kerr kama kocha mpya na anatarajiwa kuanza kazi rasmi mwanzoni mwa mwezi July.
Kocha huyo kutoka Nchini Uingereza ana uzoefu wa zaidi ya miaka 30 katika fani ya mpira wa miguu huku pia akiwa na umahiri wa kufundisha klabu mbalimbali duniani zikiwemo Hai Phong FC Vietnam, Hamilliton Academicals FC na Greennock Morton FC zote kutoka Scotland.
Kocha Kerr pia ana uzoefu wa kufundisha na kufanya kazi Afrika, ameshawahi kufanya kazi na kufundisha timu za South Africa NFD Nathi Lions FC na South Africa Thanda Royal Zulu FC kutoka Afrika Kusini

Kerr ana leseni ya daraja A na B ya ukocha aliyotunukiwa na Shirikisho la soka la Ulaya (UEFA) huku pia akiwa na uzoefu wa utawala katika fani ya michezo.
Klabu ya Simba inafuraha kubwa kuingia mkataba na kocha huyu mwenye uzoefu na weledi wa kutosha, tunaamini atakuwa chachu ya mafanikio pia kunoa vipaji vya wachezaji wa Simba.
Share:

Saturday, 20 June 2015

COPA AMERICA :URUGUAY, ARGENTINA NA PARAGUAY WATINGA ROBO FAINALI LEO NI ZAMU YA BRAZIL BILA NEYMAR

Mabingwa Watetezi Uruguay wametinga Robo Fainali za Copa America kwa Tiketi ya moja ya Timu mbili zilizofuzu Nafasi ya 3 Bora katika Kundi lao baada ya kutoka Sare 1-1 na Paraguay ambao wameshika Nafasi ya Pili ya Kundi B.
Argentina, ambao Jana waliitungua Jamaica, Timu ambayo ni Wageni Waalikwa wa Mashindano haya, Bao 1-0 kwa Bao la Dakika ya 11 la Gonzalo Higuian, wao wameshika Nambari Wani Kundi B.
Katika Mechi ya Uruguay na Paraguay, Bao la Dakika ya 29 la Jose Maria Gimenez liliwapa Uruguay uongozi lakini Dakika ya 44 Lucas Barrios aliisawazishia Paraguay.
************************
Kwenye Robo Fainali Mabingwa Uruguay watacheza na Wenyeji Chile, Argentina watacheza na Mshindi wa 3 toka Kundi C na Paraguay watacheza na Bolivia.

Leo zipo Mechi mbili za mwisho za Kundi C ambalo Timu zozote 3 kati ya 4 zinaweza kutinga Robo Fainali kwa vile zote zina Pointi 3 kila mmoja.
Brazil watacheza na Venezuela na Peru kuivaa Colombia.

Share:

SOMA HAPA TAARIFA YA TFF KUONGEZA WACHEZAJI WA KIGENI KUFIKIA 7 ,TFF YATOA NENO KUHUSU KUVURUNDA KWA TUZO

Kamati ya Utendaji ya TFF imefanya kikao chake cha kawaida leo tarehe 20/06/2015 katika ukumbi wa Wizara ya Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo kisiwani Zanzibar,
Baadhi ya maamuzi yake ni haya yafuatayo:
TUZO ZA VODACOM.
Baada ya kuzingatia mapungufu yaliyojitokeza katika uteuzi wa tuzo za ligi kuu ya Vodacom msimu wa 2014/15, Kamati ya utendaji imeagiza Rais wa TFF aunde kamati maalum ya kusimamia mchakato wa utoaji wa tuzo za Vodacom. Kamati hii itazingatia umuhimu wa kuhusisha idara za ufundi za TFF katika zoezi hilo na wadhamini na ligi watahusishwa kwa ukaribu katika zoezi hili.

KANUNI ZA LIGI 2015/16.
Kamati ya utendaji ilipitia rasimu ya kanuni za ligi kuu, FDL na SDL za msimu ujao wa 2015/16.
Mabadiliko makubwa yaliyofanywa ni kwenye maeneo yafuatayo:

LESENI ZA VILABU.
Kamati ya utendaji imesisitiza kuwa hakuna klabu itakayopitishiwa usajili wake kama kupewa leseni ya klabu ya msimu.( Club Licencing).

WAAMUZI.
Kamati ya utendaji imeridhia wazo la kamati ya maamuzi kuwa kuanzia msimu 2015/16 kutakuwa na jopo maalum ya waamuzi ( Elite referees) litakalochezeshwa mechi zote za ligi kuu.
Waamuzi hawa watakuwa ni 16 wa kati, 32 wa pembeni na 4 wa akiba. Hii itasaidia kuongoza ufanisi katika uamuzi. (refereeing).

MGAWANYO WA MAPATO YA MILANGONI.
Vilabu vimeongezwa mgawanyo wa mapato ya milangoni na sasa vitakuwa vinachukua asilimia 60% ya mapato ya mlangoni, makato mengine ni 18% VAT na 15% gharama za uwanja.


UDHIBITI WA WACHEZAJI.
Kanuni ilikuwa inatoa fursa timu ya kuamua mechi ipi mchezaji asicheze baada ya kuwa na kadi tatu za njano imefutwa.

KUSAJILI MIKATABA YA WACHEZAJI.
Kuanzia sasa mikataba kati ya wachezaji na klabu itakayotambuliwa na TFF itakuwa ni ile ambayo ni nakala halisi zilizopigwa muhuri na lakiri ya TFF na kusajiliwa kwenye kumbukumbu ya TFF. Vilabu na mwachezaji watapewa nakala hizi baada ya kusajiliwa na TFF.

WACHEZAJI WA KIGENI.
Kamati ya utendaji imeamua kuwa kuanzia msimu 2015/16 idadi ya wachezaji wa kigeni watakaosajiliwa na klabu ya ligi kuu itakuwa 7 (saba) wachezaji wote hawa, wote wataruhusiwa kucheza kwa wakati wote.
Mikakati ya kusajiliwa wachezaji hawa ni haya yafuatayo:
Mchezaji awe ni mchezaji wa timu za Taifa za nchi yake ( Senior, U23, U20, U19, U17 nk) au
Mchezaji awe anacheza katika ligi kuu ya nchi yake au nchi nyingine wakati anasajiliwa.
Kila mchezaji wa kigeni atakayesajiliwa atalipia ada ya maendeleo. Mpira wa vijana ya dola 2,000 kwa kila msimu atakyocheza hapa nchini. Fedha hizi zitapelekwa katika mfuko wa maendeleo ya mpira (Football Development Fund).
Pia imeamriwa kuwa mikataba ya vilabu na wachezaji iliyo hai itaendelea kutambuliwa na TFF. Na kwa wale ambao tayari wapo nchini wataruhusiwa kuuhisha (to renew) mikataba yao iwapo watakubaliana na vilabu vyao.

4. LESENI ZA MAKOCHA
Kamati ya utendaji imeamua kuwa kuanzia msimu huu, Kocha wa timu ya ligi kuu sharti awe na leseni B ya CAF au itakayolingana nayo kutoka katika mashirikisho mengine duniani na kocha msaidizi awe na leseni C ya CAF, hii ni kwa misimu mitatu.
Kuanzia msimu wa 2018/2019 kocha wa Ligi Kuu atatakiwa kuwa na leseni A ya CAF au inayolingana na hiyo kutoka katika mashirikisho mengine duniani.
Aidha Kamati ya Utendajji ya TFF imemteua Meshack Bandawe kuwa mjumbe wa bodi ya mfuko wa maendeleo ya mpira wa miguu – TFF (FDF), Bandawe ni meneja wa PPF kanda ya ziwa.
Share:

BAADA YA STARS KUPOKEA KIPIGO CHA MAGOLI 3-0 SASA NOOIJ KUFUNGASHIWA VIRAGO ARUDI KWAO

Taifa Stars imeendelea kuwa kichwa cha mwendawazimu baada ya kufungwa 3-0 na Uganda katika Mechi ya kwanza ya Raundi ya Awali ya kufuzu kucheza Fainali za CHAN 2016 iliyochezwa Amaan Stadium, Zanzibar Usiku wa jana.
Hadi Mapumziko, Uganda, chini ya Kocha kutoka Serbia, Milutin ‘Micho’ Sredojevic, walikuwa mbele kwa Bao 1-0 kwa Bao la Dakika ya 39 Mfungaji akiwa Erisa Sekisambu.
Kipindi cha Pili, Dakika ya 65 alikuwa tena Erisa Sekisambu aliewapa Uganda Bao lao la Pili na Bao la 3 kufungwa kwa Penati ya Farouk Miya katika Dakika ya 85.
Timu hizi zitarudiana huko Kampala baada ya Wiki mbili na Mshindi atakutana na Sudan katika Mechi ya Raundi ya Mwisho ya Mtoano na atakaeibuka kidedea ndio atatinga Fainali za CHAN 2016 zitakazochezwa Nchini Rwanda Mwakani.
******************************

Kamati ya utendaji ya Shirikishi la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Katika kikao chake cha leo pamoja na mambo mengine ilipitia mwenendo wa Timu ya Taifa (Taifa Stars) ikiwa ni pamoja na kuhudhuria mchezo kati ya Tanzania na Uganda, kama sehemu ya tathmin ya mwenendo wa timu.
Kamati ya utendaji kwa kauli moja imeamua yafuatayo:
1.Ajira ya Kocha Mkuu Maart Nooij inasitishwa mara moja kuanzia tarehe 21/June/2015.
2.Benchi lote la ufundi la Taifa stars limevunjwa kuanzia tarehe 21/06/2015.
3.Uongozi wa TFF utatangaza punde benchi jipya la ufundi la timu ya Taifa.
Share:

ANGALIA TETESI ZA SOKA ULAYA JUMAMOSI 20.06.2015 KUTOKA MAGAZETI MBALIMBALI YA MICHEZO

Liverpool wamemsajili beki anayetajwa kuwa na kipaji Joe Gomez, 19, kutoka Charlton kwa pauni milioni 3.5. Mchezaji huyo wa kimataifa wa England chini ya miaka 19, amefanya vipimo vya afya siku ya Ijumaa na kusaini mkataba wa miaka mitano. Gomez, ataungana na Liverpool katika mechi za kabla ya kuanza msimu, lakini anatarajiwa kwenda kucheza kwa mkopo, na Derby wanadhaniwa kumtaka. "Ndoto yangu imekuwa kweli. Siamini bado. Lakini nina furaha sana" amesema Gomez.
******************************************
Manchester City watatoa pauni milioni 40 kumtaka kiungo wa Arsenal Jack Wilshere, 23, iwapo watashindwa kumpata Paul Pogba, 22 kutoka Juventus kwa pauni milioni 70 (Daily Star),
******************************************
Meneja wa Juventus Massimiliano Allegri ana uhakika Juve watamshikilia Pogba na hawana shinikizo lolote la kumuuza (Sun), winga Angel Di Maria, 27, amesema alipata tabu msimu wa kwanza Man Utd kwa sababu Kombe la Dunia lilikuwa gumu alipoichezea Agentina (Tovuti ya Copa America),
*******************************************
Beki kutoka Argentina Nicolas Otamendi, 27, anayenyatiwa na Manchester United amedokeza kuwa huenda akaondoka Spain baada ya kusema klabu yake ya Valencia "inafahamu anachotaka" (Metro),
*******************************************
 Liverpool wanafikiria kutaka kumchukua kiungo wa Hoffenheim Roberto Firmino, 23, ambaye anatakiwa pia na Manchester United Daily (Mirror), Arsenal wametoa dau la pauni milioni 28.5 kumtaka kiungo wa Sporting Lisbon William Carvalho na huenda wakaongeza kiasi hicho kwa pauni milioni 8.5 ili kutengua kipengele cha uhamisho wake (Sun),
*******************************
 kuondoka kwa kocha wa makipa wa Arsenal Tony Roberts kumeongeza tetesi kuwa kipa wa Chelsea Petr Cech kujiunga na Gunners akienda na kocha wake (Independent), 
*****************************************
Chelsea wamehusishwa na mshambuliaji wa Atletico Madrid Antoinne Griezmann, lakini PSG wametoa dau la pauni milioni 28.5 kumtaka mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa ambaye ana kipengele cha uhamisho cha pauni milioni 43 kwenye mkataba wake 
Share:

COPA AMERICA: CHILE NA BOLIVIA WAPATA USHINDI NA KUSONGA MBELE ROBO FAINALI

Wenyeji Chile na Bolivia wametinga Robo Fainali za Copa America baada ya kushinda Mechi zao za mwisho za Kundi A Jana Usiku.
CHILE 5-0 BOLIVIA
Wakicheza Estadio Nacional de Chile Mjini Santiago, Chile waliibamiza Bolivia 5-0 kwa Bao za Charles Aranguiz, Dakika za 3 na 79, Alexis Sanchez, 66,  Gary Medel, 86, na Ronald Raldes kujifunga mwenyewe.
Licha ya Bolivia kupata kipigo hicho, wao wamefuzu kutinga Robo Fainali kwa kumaliza Nafasi ya Pili.
Nao Ecuador wametwaa Nafasi ya 3 ya Kundi A baada ya kuichapa Mexico 2-1 na wanangojea Makundi mengine kumaliza Mechi zao na kujua kama wataingia Robo Fainali kwa Tiketi moja kati ya mbili za Mshindi wa Tatu Bora toka Makundi yote Matatu.
MEXICO 1-2 ECOADOR
Bao za Ecuador kwenye Mechi hiyo zilifungwa na Miler Bolanos na Luis Antonio Valencia katika Dakika za 56 na 67 na Mexico kupata Bao lao moja kwa Penati ya Dakika ya 64 iliyopigwa na Raul Jimenez.
Leo zipo Mechi mbili za mwisho za Kundi B ambpao Vigogo Argentina watacheza na Timu Mwalikwa Jamaica na Mabingwa WAtetezi Uruguay kukipiga na Paraguay.
MSIMAMO:
KUNDI A
1 Chile Pointi 7
2 Bolivia 4
3 Ecuador 3
4 Mexico 2
KUNDI B
1 Argentina Pointi 4
2 Paraguay 4
3 Uruguay 3
4 Jamaica 0
KUNDI C
1 Peru Pointi 3 
2 Brazil 3
3 Colombia 3
4 Venezuela 3 
********************************************
COPA AMERICA MICHEZO YA LEO
Jumamosi Juni 20
KUNDI B Uruguay v Paraguay (Saa 4 Usiku)
KUNDI B Argentina v Jamaica (Saa 6 na Nusu Usiku)

Share:

NEYMAR AFUNGIWA MECHI 4 NDO BASI TENA COPA AMERICA

Shirikisho la Soka la Nchi za Marekani ya Kusini, CONMEBOL, limemfungia Kepteni wa Brazil Neymar Mechi 4 na hivyo kumtupa nje ya Copa America ambayo Brazil inashiriki.
Kifungo hiki kinamaanisha Neymar ataikosa Mechi ya mwisho ya Brazil ya Kundi C la Copa America na pia Robo Fainali na Nusu Fainali ikiwa Brazil itafuzu.
Juzi, CONMEBOL awali ilimfungia Neymar Mechi 1 baada ya kupewa Kadi Nyekundu Jumatano wakati Brazil inachapwa 1-0 na Colombia katika Mechi ya Kundi C la Copa America huko Nchini Chile.
Kifungo hicho kilimfanya Neymar kuikosa Mechi ya mwisho ya Kundi C watayocheza Jumapili dhidi ya Venezuela Mechi ambayo ni muhimu mno kwao kufuzu kutinga Robo Fainali kwani Timu zote za Kundi hilo zimefungana zikiwa na Pointi 4 kila mmoja.
Hata hivyo, wakati huo, Neymar alikuwa tayari aikose Mechi hiyo na Venezuela kwani alikuwa ameshazoa Jumla ya Kadi za Njano mbili katika Mashindano hayo.
Katika Mechi hiyo na Colombo, Neymar alionyeshwa Kadi Nyekundu na Refa wa Chile Enrique Osses Mpira ukiwa umekwisha baada kumbabatiza na Mpira Mchezaji wa Colombia Pablo Armero kitu ambacho kilizua rabsha na Neymar kuonekana akijaribu kumpiga Kichwa Mchezaji mwingine wa Colombia.
Katika rabsha hizo, Mchezaji wa Colombia, Carlos Bacca, nae alipewa Kadi Nyekundu.
CONMEBOL ikitangaza Kifungo hiki cha Neymar imetamka kuwa wote, Neymar na Bacca, wana haki ya kukata Rufaa.
Mwaka 2014, huko Nchini kwao Brazil, Neymar alilazimika kuondoka kwenye Fainali za Kombe la Dunia na kukosa Mechi zilizobakia baada ya kupigwa Goti Mgongoni na Mchezaji wa Colombia Juan Zuniga na kuvunjwa Mfupa wa Mgongoni bila ya huyo Zuniga kuadhibiwa.
 
Share:

HABARI ZA USAJILI TANZANIA LEO KUBWA OKWI KUONGEZEWA MKATABA ,KASEJA ARUHUSIWA KUSAJILIWA TIMU YOYOTE HUKU KESI IKIENDELEA

UONGOZI wa klabu ya Azam FC upo katika hatua ya mwisho kumnasa kiungo wa kimataifa wa APR ya Rwanda, Jean Baptiste Mugiraneza, ili kuwadhibiti washambuliaji machachari wa timu za Ligi Kuu Tanzania Bara, wakiwamo Warundi Amissi Tambwe na Laudit Mavugo, anayewaniwa na Simba na wengineo.
Tayari mazungumzo baina ya mchezaji huyo na Azam FC yamefikia pazuri na kwamba kilichobaki ni kusaini mkataba wa kukitumikia kikosi hicho chenye maskani yake Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
*********************************




Nyota wa Simba, Emmanuel Okwi amebakisha miezi sita tu kuitumikia timu yake na sasa anajadiliana na timu yake kuhusu kuongeza mkataba baada ya Yanga kumwambia: “Noo, haiwezekani.”
Yanga wanadai Okwi baada ya kuona yupo huru kuzungumza na timu yoyote kuhusu usajili wake, akaamua kujaribu kwa kuzungumza na Wanajangwani lakini hawakuweza kufika mbali mapema wakashindwana ndipo aliporudi Simba.

**********************************
Mtibwa Sugar wala haina kinyongo na sasa ipo katika mchakato wa kuwarejesha wachezaji wake walioachwa na Simba na Yanga ili waanze upya harakati zao za soka
Muda wowote kuanzia sasa Mtibwa ya Turiani, Morogoro itakuwa imeshawarejesha beki wa kushoto Issa Rashid ‘Baba Ubaya’ kutoka Simba na straika Said Bahanuzi kutoka Yanga. Pia imepanga kumsajili Haruna Chanongo aliyemaliza mkataba Simba.
********************
Mwadui FC ya Shinyanga haitaki mchezo na imesema tayari imemsajili beki wa kati David Mwantika aliyemwagwa Azam FC, usibishe.
Awali, Mwantika alifanya mazungumzo na Simba mara mbili lakini wakaonekana kutopatana vizuri.
*********************


****************************
Yanga imesema haina sababu zozote za kumzuia kipa Juma Kaseja kujiunga na timu nyingine kwa kuwa kweli haimhitaji.
Awali kulikuwa na taarifa kwamba Yanga inamfanyia Kaseja ntomanyongo kwa kushindwa kumuachia aende timu nyingine.
Lakini Mwanasheria wa Yanga, Frank Chacha amesema Kaseja yuko huru kujiunga na timu nyingine wakati kesi yao dhidi yake ikiendelea.
Share:

LEO USIKU ZANZIBAR NI STAR VS UGANDA HATMA YA NOOIJ KUJULIKANA KAMA ANBAKI AU ANONDOKA

Kocha wa Timu ya Taifa ya Tanzania Mart Nooij Leo anaanza mtihani wake wa kwanza wa kulinda kibarua chake wakati Taifa Stars itakaposhuka Amaan Stadium, Zanzibar kucheza na Uganda katika Mechi ya kwanza ya kufuzu Fainali za CHAN.Embedded image permalink
Tangu Kocha huyo kutoka Holland achukue Timu Mwaka Jana, Stars imeshinda Mechi 3 tu na kubamizwa 8 katika Mechi zake 17 kitu ambacho kimeamsha hasira za Washabiki ambao wengi wao wanataka atimuliwe.
Mwezi uliopita, Stars ilialikwa huko Afrika Kusini kucheza COSAFA CUP na kufungwa Mechi zao zote 3 za Kundi lao na Wiki iliyopita ilikuwa huko Borg Al Arab na kupigwa 3-0, Bao zote ndani ya Dakika 9, na Misri katika Mechi yao ya kwanza ya Kundi lao la AFCON 2017.
Hali hii ilizua tafrani Jijini Dar es Salaam kiasi baadhi ya Watu kufanya uhuni wa kulipiga mawe Basi la Taifa Stars kitendo ambacho kinalaaniwa sana.
Hata hivyo, TFF imetoa tamko rasmi kuwa wataachana nae Mart Nooij pale tu akishindwa kuifikisha Taifa Stars Fainali za CHAN 2017 zitakazochezwa Mwakani huko Rwanda.
CHANI ni Mashindano ya Timu za Taifa za Afrika kwa Wachezaji wale tu wanaochezea Soka lao ndani ya Nchi zao tu.
Share:

Sunday, 14 June 2015

ANGALIA KIKOSI CHA STARS KITAKACHOWAVAA MISRI LEO USIKU

Kikosi cha leo cha Taifa Stars Vs Misri


1 Munishi
2 Kapombe
3 Oscar
4 Haroub
5 Morris
6 Nyoni
7 Kazimoto
8 Kiemba
9 Samatta
10 Ulimwengu
11 Mkude

Benchi
1 Mwadini
2 Mwinyi H
3 Mbonde
4 Domayo
5 Bocco
6 Msuva

Share:

Thursday, 11 June 2015

MSUVA AIBUKA MCHEZAJI BORA KADO GOLIKIPA BORA MTIBWA WAPATA SIFA YA KUWA NA NIDHAMU GORAN, HANS VAN DER HOI

KOCHA BORA-----MBWANA MAKATA (PRISONS)... Amenyakua milioni 8

MCHEZAJI BORA....SAIMON MSUVA (YANGA)...Amenyakua milioni 5

GOLIKIPA BORA...SHABAN HASSAN KADO (COASTAL UNION)---Amenyakua milioni 5

MWAMUZI BORA....ISRAEL MUJUNI NKONGO

TIMU YA NIDHAMU....MTIBWA SUGAR FC

Vipengele vilivyokuwa vikishindaniwa ni hivi hapa chini, muda si mrefu tutakuletea orodha nzima ya zawadi.


1. Mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom 2014/2015
  1.  Mohamed Hussein (Simba SC)
  2.  Mrisho Ngasa (Young Africans)
  3.  Saimon Msuva (Young Africans)

2. Mlinda mlango bora wa Ligi Kuu ya Vodacom 2014/2015
  1. Mohamed Yusuph (Tanzania Prisons)
  2. Said Mohamed (Mtibwa Sugar)
  3.  Shaban Hassan (Coastal union)

3. Kocha bora wa Ligi Kuu ya Vodacom 2014/2015
  1. Goran Kopunovic (Simba SC)
  2.  Hans Van Der Pluijm (Young Africans)
  3.  Mbwana Makata - (Tanzania Prisons)

4. Mwamuzi bora wa Ligi Kuu ya Vodacom 2014/2015
  1. Israel Mjuni Nkongo
  2.  Jonesia Rukyaa
  3.  Samwel Mpenzu

5. Timu yenye nidhamu Ligi Kuu ya Vodacom 2014/2015
  1. Mgambo JKT
  2.  Mtibwa Sugar
  3.  Simba SC
Share:

COPA AMERIKA UFUNGUZI LEO USIKU MECHI YA KWANZA NI CHILE VS ECUADOR

COPA AMERICA 2015, Kombe la Mataifa ya Marekani ya Kusini, linaanza Leo Usiku huko Nchini Chile ambapo Wenyeji hao watafungua dimba Mechi ya Kundi A kwa kupambana na Ecuador.
Hapo kesho itakuwepo Mechi nyingine ya Kundi A kati ya Wageni Waalikwa Mexico watakapocheza na Bolivia.
Jumamosi zipo Mechi mbili za Kundi B kati ya Mabingwa Watetezi Uruguay na Timu nyingine Waalikwa, Jamaica, na kufuatiwa na Mechi kati ya Argentina na Paraguay.
Jumapili Mechi za kwanza za Makundi zitakamilika kwa Mechi mbili za Kundi C wakati Brazil watakapoivaa Peru na Colombia kucheza na Venezuela.
Share:

MECHI ZA KIRAFIKI KIMATAIFA: UJERUMANI IMECHAPWA 1-0 NA MAREKANI, BRAZIL FULL USHINDI

Tangu wachukue Kombe la Dunia Mwaka Jana na njiani kwake kuifedhehesha vibaya Brazil, Germany wameendelea mwendo mbovu baada ya Jana kufungwa na USA huko Bremen wakati Brazil, wakicheza Nchini kwao, kuichapa Honduras na kuendeleza wimbo lao la ushindi wa Mechi 10 mfululizo chini ya Kocha Dunga.

Huko Weserstadion, Bremen, Germany walitangulia kuifunga USA Bao 1-0 katika Dakika ya 12 kupitia Mario Gotze lakini USA kuzinduka na kupiga Bao 2 katika Dakika za 41 na 87 kupitia Mix Diskerud na Bobby Wood na kujizolea ushindi wa 2-1 chini ya Kocha wao Mjerumani Jurgen Klinsman.
Huko Porto Allegre, Brazil, Bao la Dakika ya 33 la Mshambuliaji wa Hoffenheim, Roberto Firmino, ambae sasa ndio nyota mpya ya Brazil, liliwapa ushindi wa Bao 1-0 walipocheza na Honduras.
Juzi Brazil, wakicheza huko Sao Paulo, waliifunga Mexico 2-0.
Tangu Dunga ashike wadhifa wa Kocha wa Brazil baada Nchi hiyo kufanya vibaya katika Kombe la Dunia Mwaka Jana, Brazil imeshinda Mechi 10 mfululizo na sasa inakwenda Nchini Chile kushiriki Copa America.
Share:

ORODHA YA WANAMICHEZO 10 WANAOONGOZA KWA FEDHA NYINGI DUNIANI BONDIA MAYWEATHER NDO NAMBARI 1

Bondia Floyd Mayweather ni mwanamichezo anayeongoza kwa kulipwa fedha nyingi katika kipindi cha miezi 12 iliyopita. Hii ni kwa mujibu wa jarida la biashara la Forbes. Orodha ya kila mwaka ya wanamichezo matajiri imeonesha Mayweather, aliyekuwa akiongoza pia mwaka jana, anaongoza tena mwaka huu kwa kujipatia dola milioni 300.
 Fedha nyingi kati ya hizo zimetokana na 'mpambano wa karne' dhidi ya Manny Pacquiao, ambaye kipato chake cha dola milioni 160 kinamfanya kuwa nafasi ya pili katika orodha hiyo. Mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo ameshika nafasi ya tatu akiwa na dola milioni 79.6.  

1. Floyd Mayweather, Marekani, Ndondi = US$300m (£194m).
2. Manny Pacquiao, Ufilipino, Ndondi = $160m (£103.4m)
3. Cristiano Ronaldo, Ureno, Soka = $79.6m (£51.4m)
4. Lionel Messi, Argentina, Soka = $73.8m (£47.7m)
5. Roger Federer, Uswisi, Tennis = $67m (£43.3m)
6. LeBron James, Marekani, Mpira wa Kikapu = $64.8m (£41.9m)
7. Kevin Durant, Marekani, Mpira wa Kikapu = $54.1m (£35m)
8. Phil Mickelson, Marekani, Gofu = $50.8m (£32.8m)
9. Tiger Woods, Marekani, Gofu = $50.6m (£32.7m)
10. Kobe Bryant, Marekani, Mpira wa Kikapu = $49.5m (£32m)
Share:

TAIFA STARS KESHO INAONDOKA KUELEKEA MISRI

Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premier Lager, kesho siku ya ijumaa jioni inatarajiwa kuondoka Addis Ababa Ethiopia kuelekea nchini Misri tayari kwa mchezo wa siku ya jumapili.
Stars ambayo imeweka kambi ya mazoezi takribani kwa wiki moja sasa jijini Addis Ababa leo imeendelea na raiba yake ya mazoezi katika uwanja wa Taifa, amabpo leo imefanya mazoezi yake asububuhi tu.
Kocha mkuu wa T
aifa Stars Mart Nooij amesema, anashukuru maendeleo ya kambi ni mazuri timu yake inafanya mazoezi katika viwanja viwili vizuri vilivyopo Addis Ababa, uwanja wa Taifa na  uwanja wa Benki ya Biashara ya Ethiopia.
Nooij amesema amekuwa akiwafundisha wachezaji wake kucheza mpira wa kasi na pasi za haraka haraka, jambo ambalo wachezaji wameonyesha kufuata vizuri maelekezo yake na kusema wanamuelewa vizuri.
Akiongelea mchezo dhidi ya Misri siku ya jumapili, Nooij amesema timu inakwenda kupambana kusaka matokeo mazuri katika mchezo, nafahamu tunaenda cheza ugenini, nimewaelekeza vijana wangu wanaocheza nafasi ya ushambuliaji kutumia vizuri nafasi tutakazozipata katika mchezo huo.
Aidha kocha Nooij amesema katika mpira hakuna kinachoshindikana, kambi ya wiki moja Addis Ababa imewasaidia wachezaji kukaa pamoja na kushika maelekezo yake vizuri, hivyo anaamini timu yake itafanya vizuri katika mchezo huo wa kuwania kufuzu kwa fainali za AFCON. 
Share:

Friday, 5 June 2015

SIMBA SC KUMFIKISHA RAMADHANI MESSI KWENYE VYOMBO VYA DOLA

Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
UONGOZI wa Simba umesema umeamua kulifikisha polisi sakata la usajili wa kiungo mshambuliaji Ramadhani Singano 'Messi' ili kulinda taswira ya klabu hiyo.
Messi anadai kutotambua uhalali wa mkataba wake wa miaka mitatu na Simba uliopo katika Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) huku akisisitiza ana mkataba wa miaka miwili na klabu hiyo ya Msimbazi utakaomalizika Julai Mosi mwaka huu.
Hajji Manara, msemaji wa Simba, katika mahojiano na moja ya vituo vya redio jijini hapa leo, amesema kuwa kutokana na mvutano ulioibuka baina ya pande zote mbili, klabu imeona ni vyema kulifikisha suala hilo mbele ya vyombo vya dola ili lipatiwe ufumbuzi.

"Simba ni taasisi kubwa, suala hili linachafua 'image' (taswira) ya taasisi hii. Tukumbuke pia kwamba Simba ina wadhamini. Inaposdemwa kwamba tumeghushi nyaraka likiwamo dole gumba la Messi, ni kashfa kubwa. Wadhamini wanatuelewaje?" Amehoji Manara bila kutaja lini hasa suala hilo litatinga polisi.
Wakati Simba wakitishia kulifikisha suala hilo mikononi mwa polisi, tayari Chama cha Wachezaji wa Soka Tanzania (Sputanza) kimeshalifikisha sakata hilo mikononi mwa TFF ili litatuliwe na Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya shirikisho hilo.

Mwenyekiti wa Sputanza, Mussa Kisoky, alisema jijini jana kuwa walifikia hatua ya kuonana na uongozi wa TFF baada ya kupewa maelezo na winga huyo mwenye umri wa miaka 21.
Share:

AZAM KUSAJILI WACHEZAJI KONGO MBWANA SAMATA AOMBWA KUWASAIDIA

Hatimaye sasa Azam FC nayo imeanza kutanua makucha na tayari imetua kwenye timu maarufu Afrika, TP Mazembe ya DR Congo na kutaka saini za wachezaji wawili hatari wa timu hiyo.
Taarifa makini zilizopatikana kutoka kwa mmoja wa mabosi wa ngazi ya juu Azam, zimebainisha mpango huo wa kuwataka wachezaji hao raia wa DR Congo walio kwenye kikosi cha kwanza cha Mazembe ambao mmojawao anamudu nafasi ya beki wa kulia na mwingine ni straika.

Chanzo hicho kimefafanua kuwa imekuwa ngumu kuwashawishi wachezaji hao na sasa wamemua kumtumia mshambuliaji wa timu hiyo, Mtanzania, Mbwana Samatta ambaye alikubali na ameonyesha kupata mafanikio makubwa katika kukamilisha zoezi hilo.
Taarifa zinaeleza kwamba awali wachezaji hao ambao mpaka sasa majina yao bado ni siri, walikuwa wagumu walipoelezwa suala la kuhama Congo na kuja kukipiga Tanzania lakini baadaye baada ya kushirikishwa Samatta ambaye ni straika tegemeo wa timu hiyo, sasa mambo yameanza kulainika na mchakato unakwenda vizuri.
“Kuna wachezaji kwa sasa tunawatafuta kwa ajili ya kuweka mambo sawa msimu ujao na kuzidi kusonga mbele zaidi ya hapa tulipo sasa, tayari kuna harakati za kumpata beki mmoja wa kulia na mwingine ni straika, wote raia wa Congo.
“Wanacheza TP Mazembe, tuliamua kumtumia Samatta kwa kuwa awali ilikuwa ngumu kuwapata,” alisema bosi mmoja wa Azam.
Alipoulizwa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba, juu ya suala hilo alikana na kusema: “Hakuna suala kama hilo.”

SOURCE: CHAMPIONI
Share:

HABARI ZA USAJILI BONGO: SOMA HAPA KWANINI NYOTA WA MBEYA CITY WANAIHAMA KLABU HIYO

Imefahamika kuwa maslahi madogo yaliyopo kwenye Klabu ya Mbeya City ndiyo sababu kubwa ya wachezaji nyota kuikimbia timu hiyo.
Mbeya City ambayo imekuwa na jina kubwa ndani ya misimu miwili iliyocheza Ligi Kuu Bara, imekimbiwa na wachezaji wanne waliokuwa katika kikosi cha kwanza ambao ni Peter Mwalyanzi aliyetua Simba, Deus Kaseke (Yanga), Paul Nonga na Anthony Matogolo (Mwadui FC).

Nonga ambaye ametua Mwadui na kupewa mkataba wa mwaka mmoja, amesema kilichomuondoa ni maslahi na hakuwa na jinsi.
“Mwadui wamenipa dau zuri zaidi ya lile la Mbeya City. Mpira ndiyo kazi yangu, hivyo naangalia maslahi na si kingine,” alisema Nonga.
Ikumbukwe kuwa dirisha la usajili bado halijafunguliwa na kuna uwezekano wa wachezaji zaidi kuihama timu hiyo ambayo nayo imewasajili Gideon Brown aliyetokea Ndanda, Haruna Shamte (JKT Ruvu) na Joseph Mahundi (Coastal Union).
Share:

MNCHESTER UNITED NDIO TIMU INAYOINGIZA PESA NYINGI ZAIDI UINGEREZA ANGALIA LISTI YA TIMU 10 TAJIRI

Wakati Ligi Kuu England ikizidi kutajirika kwa kuongeza Mapato yake kwa Asilimia 29 na kufikia Pauni Bilioni 3.3, Manchester United ndiyo inayoongoza kwa kuwa na Mapato ya juu kabisa.
Mahesabu hayo yametolewa na Magwiji wa ushauri wa Kifedha Duniani, Deloitte, ambao wamesema Man United ipo juu kwa kuvuna Pauni Milioni 433.2 kwa Mwaka wa Fedha wa 2013/14.
Deloitte imesema Klabu zilizopiga hatua kubwa katika kipindi hicho ni Everton, Aston Villa na Chelsea lakini Man United imeendelea kuwa juu.
Deloitte imesema kukua kwa Mapato hayo kumetokana hasa na kuongezeka kwa Mapato yatokanayo na Matangazo ya TV

LISTI YA MAPATO 2013/14:
1.Man United £433.2m

2.Man City £348.3m

3.Chelsea £324.4m

4.Arsenal £300.5m

5.Liverpool £255.8m

6.Tottenham £180.5m

7.Newcastle £129.7m

8.Everton £120.5m

9.West Ham £116.5m

10.Aston Villa £111.2m


Share:

KESHO NI FAINALI YA UEFA BARCA AU JUVE PATA TATHIMINI CHIELINI KUIKOSA MECHI HII

Hii ni Fainali ya UEFA ambayo ama FC Barcelona ya Spain au Juventus ya Italy itatwaa Ubingwa wa Ulaya na pia Bingwa huyo atakuwa ametwaa Trebo Msimu huu baada ya Timu zote mbili kutwaa Makombe mawili Nchini mwao yale ya Ubingwa na Kombe la Nchi.

Habari kubwa ya Fainali hii ni kukosekana kwa ule mvuto mkubwa wa kuwakutanisha tena kwa mara ya kwanza Beki wa Juventus Giorgio Chiellini na Fowadi wa Barcelona Luis Suarez baada ya Chiellini kuumia Jumatano.
Wachezaji hao walivaana huko Brazil Mwaka Jana wakizichezea Nchi zao kwenye Fainali za Kombe la Dunia na Suarez kuadhibiwa kwa Kifungo kirefu kwa kumng'ata Meno Chiellini.
HALI ZA VIKOSI VYOTE:

************JUVENTUS
Timu inayotarajiwa kuanza:
Buffon; Lichtsteiner, Bonucci, Barzagli, Evra; Marchisio, Pirlo, Pogba; Vidal; Tévez, Morata.
Majeruhi: Barzagli, Chiellini, Cáceres
BARCELONA
Timu inayotarajiwa kuanza:
Ter Stegen; Alves, Piqué, Mascherano, Alba; Rakitić, Busquets, Iniesta; Messi, Suárez, Neymar.
Majeruhi: Hamna
REFA: CUNEYT CAKIR [TURKEY
Share:

Monday, 1 June 2015

MCHEZAJI WA KUTEGEMEWA WA NDANDA GIDEON BENSON AMESAINI MBEYA CITY HII LEO

Mshambuliaji wa kutumainiwa wa ndanda Fc, Gidion Brown amesaini kandarasi mpya ya mwaka mmoja na nusu kujiunga na kikosi Mbeya City fc kinachonolewa na Juma Mwambusi katika msimu ujao huku akiweka kando ofa kadhaa alizopata kutoka vilabu mbalimbali vinavyoshiriki ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara alizopata hapo kabla.


Akizungumza mara baada ya kusaini kandarasi hiyo mapema leo kwenye ofisi za Mcc fc zilizopo Mkapa Hall jijini Mbeya, Brown alisema kuwa limekuwa jambo zuri kwake kujiunga na timu ambayo inaweza kumpa mafanikio nje na klabu zingine zilizozoeleka.



“Watu wengi wengi wanaamini kuwa huwezi kufanikiwa bila kupita kule, binafsi nahisi ni tofauti kwa sababu kipaji kinaweza kuonekana popote,imani yangu nitafanikiwa hapa, City ni timu nzuri na ina mipango ya ya kweli, nataka kufanya kazi kwa kiwango kikubwa na imani yangu sitawaangusha wale wote wenye mapenzi na timu hii, najaua nitakuwa chini ya mwalimu Mwambusi, huyu ni kocha ambaye siku zote nimekuwa na kiu ya kufanya nae kazi, hili limetimia sasa” alisema mshambuliaji huyo.



Msimu uliopita Brown alikuwa moja ya wachezaji muhimu kwenye kikosi cha Ndanda Fc akicheza michezo 21 akiwa kwenye kikosi cha kwanza, na kuifungia timu hiyo ya Mtwara jumla ya mabao 5, awali mshambuliaji huyu amewahi kukupiga kwenye timu za KMKM ya Zanzibar na kuisaidia kutwaa taji la ligi kuu ya visiwani humo pia amecheza kwenye kikosi cha Rhino ya Tabora na Moro United.

Share:

ANGALIA TETESI ZA USAJILI BONGO KUBWA KOCHA WA YANGA KUJA NA WACHEZAJI TOKA GHANA NAO AZAM WAWATEMA WACHEZAJI WANNE

Pamoja na kumsaini winga , Deus Kaseke na straika Malimi Busungu, bado Yanga wamesema hawajaridhika zaidi, hivyo wanataka kuongeza nguvu kwenye wingi zote- kulia na kushoto.
Katika kufanikisha hilo, Kocha Mkuu, Hans van Der Pluijm, anatarajiwa kushuka Bongo ndani ya wiki hii ambapo ataambatana na wachezaji wawili wanaomudu wingi ya kulia na kushoto.
Habari kutoka Yanga zinasema kuwa lilikuwa pendekezo la kocha mwenyewe, lakini taarifa nzuri kwa Wanayanga ni kwamba nyota hao ni kama mapacha- wanajuana kwa kina, kwani wote wanatokea timu moja inayoshiriki ligi kuu nchini Ghana.

******************
Beki mpya aliyesajiliwa na Simba hivi karibuni akitokea JKT Ruvu, Mohammed Faki, amekwaa kisiki katika kikosi hicho cha Wanamsimbazi, baada ya jezi ya namba aliyokuwa akiihitaji kuwa na mtu.
Faki amesajiliwa na Simba kwa mkataba wa miaka miwili ambapo alikuwa akiihitaji jezi yenye namba 26 ambayo alikuwa akiivaa tangu alipokuwa Ashanti United na JKT Ruvu, lakini katika kikosi cha Simba, inavaliwa na nahodha, Hassan Isihaka.
Faki amesema kwa kuwa bado hajakabidhiwa jezi tangu asajiliwe Jumatano ya wiki iliyopita, lakini kama angekuta jezi namba 26 haina mtu, basi ingekuwa mali yake.
******************
Kwa mujibu wa ukurasa wa facebok wa Azam FC ni kwamba, Azam FC imewaruhusu wachezaji wake watatu waliomaliza mikataba yao kutafuta timu nyingine
Wachezaji hao ni Gaudence Mwaikimba, Amri Kiemba (mkopo toka Simba) na Wandwi Jackson
Pia klabu imerefusha mikataba ya wachezaji waliokuwa wakikaribia kumaliza mikataba yao. Wachezaji hao ni Said Morad, Erasto Nyoni, Dedier Kavumbagu, Khamis Mcha, Waziri Salum, Brison Raphael, Joseph Kimwaga, Mudathir Yahya na Farid Mussa.
Share:

TAIFA STARS YAINGIA KAMBINI LEO KUWAWINDA MISRI ANGALIA KIKOSI KAMILI

Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) ambayo inadhaminiwa na kampuni ya bia ya Kilimanjaro, leo inaingia kambini katika hoteli ya Tansoma iliyopo eneo la Gerezani kujiandaa na mchezo dhidi ya Misri kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika (AFCON).
Kikosi kitakachoingia kambini kinawajumuisha wachezaji waliocheza michuano ya Cosafa nchini Afrika Kusini mwishoni mwa mwezi Mei, wachezaji 20 walioanza kambi tangu wiki iliyopita na wachezaji wanaocheza soka la kulipwa nchini Congo DR.

Taifa Stars inatarajiwa kufanya mazoezi katika uwanja wa Gymkana na Uwanja wa Taifa kwa muda siku mbili kabla ya siku ya alhamis kusafiiri kuelekea Addis Ababa nchini Ethiopia ambapo itaweka kambi ya wiki moja kujiandaa na mchezo dhidi ya Misri.
Wachezaji wanaotarajiwa kuingia kambini leo ni Deogratias Munish, Mwadini Ali, Shomari Kapombe, Oscar Joshua, Haji Mwinyi, Aggrey Morris, Salum Mbonde, Erasto Nyoni, Saimon Msuva, Hassan Dilunga, Joram Mgeveke, Juma Liuzio, Said Ndemla, Mwinyi Kazimoto, Abdi Banda, John Bocco, Mrisho Ngasa, Salum Abubakar, Ibrahim Hajibu, Thomas Ulimwengu na Mbwana Samatta.

Wachezaji waliopo kambini tangu wiki iliyopita ni Nadir Haroub, Juma Abdul, Salum Telela, Peter Manyika jr, Jonas Mkude, Hassan Isihaka, Mohamed Hussein, Aishi Manula, Frank Domayo, Mudathir Yahya, Kelvin Friday, Malimi Busungu, Bennedict Tinoco, Rashid Mandawa, Atupele Green, Haroun Chanongo, Emmanuel Simwanda, Said Mohamed, Andrew Vicent, Gadiel Michael, Deus Kaseke.
Msafara wa Taifa Stars unatarajiwa kuondoka nchini Alhamis Juni 4, 2015 kuelekea Ethiopia ukiwa na wachezaji 23,benchi la ufundi pamoja na viongozi .Mechi kati ya Misri dhidi ya Tanzania inatarajiwa kuchezwa Juni 14, 2015 katika uwanja wa Borg El Arab pembeni kidogo ya jiji la Alexandria.
Wakati huo huo Tanzania imepata mwaliko wa kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya Taifa ya Rwanda kati ya Juni 6, 7 mwaka huu jijini Kigali, kwenye kumbukumbu ya mauaji ya kimbali, Tanzania itapeleka kikosi cha vijana U23 katika mchezo huo utakaochezwa mwishoni mwa wiki.
Kufuatia kupata mwaliko huo kikosi cha U23 kitaondoka nchini ijumaa tarehe 5, Juni 2015 kuelekea nchini Rwanda kikiwa na wachezaji 18 chini ya kocha Salum Mayanga.
Kocha wa Mtibwa Sugar Mecky Maxime ameongezwa kwenye benchi la ufundi litakalokwenda Ethiopia kisha nchini Misri kufuatia kocha Salum Mayanga kuwa na timu ya U23 nchini Rwanda.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
Share:
Powered by Blogger.

IDADI YA WANAOTEMBELEA BLOG HII

Blog Archive

Recent Posts

Fashion

3/Fashion/big-col-right

Recent Posts

Header Ads

Followers

Powered By Blogger

Tags

Maoni

3/recent-comments

WASILIANA NASI

Popular Posts

Labels

Blog Archive

Blogger templates