Pages

Thursday, 17 May 2018

MICHEZO : LIPULI YAGOMEA SALAMBA KWENDA YANGA

Timu ya Lipuli ya Iringa imejibu barua ya Yanga iliyomtaka Adam Salamba kuichezea Yanga ili kuisaidia katika michezo ya kimataifa

BARUA YA LIPULI KWA YANGA HII HAPA



Share:

BURUDANI : WIZKID STAR BOY NA KASHFA YA KUTELEKEZA MTOTO

Nyota wa muziki kutokea Nigeria Wizkid “Starboy” amelalamikiwa kupitia mitandao ya kijamii baada ya mwanamke aliyezaa nae mtoto wake wa pili Binta Diamond Diallo kutoa malalamiko kupitia ukurasa wake wa instagram kuwa staa huyo hatoi matunzo kwa mtoto wake.
Kupitia ukurasa wa instagram wa Binta ambaye ni mwanamke aliyezaa na Wizkid ameandika
 “Sijali ulipo, sijali upo na nani, kama una watoto hakikisha unawajali na unapata muda wa kuwa nao #usitoevisingizo”
Share:

MICHEZO : MKONGWE BUFFON ATANGAZA RASMI KUVUA GLOVU

Kipa Gian Buffon ametangaza ataondoka katika klabu ya Juventus mwishoni mwa msimu huu baada ya kuwa hapo kwa miaka 17.

REKODI ZA BUFFON HIZIZ HAPA

Share:

MICHEZO : ATLETICO MADRID MABINGWA WA EUROPA LIGI WAKISHINDA 3-0 DHIDI YA MARSEILLE

Antoine Griezmann alifunga mabao mawili na kuwawezesha Atletico Madrid kuwachapa Marseille 3-0 mjini Lyon, Ufaransa na kushinda Kombe la Europa League mara yao ya tatu katika kipindi cha miaka tisa.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa alianza kwa kufunga baada ya Andre Zambo Anguissa kutomakinika na mpira dakika ya 21 na kisha akafunga la pili dakika ya 49.
Nahodha wao Gabi alifunga bao la tatu dakika ya 89 na kuwawezesha vijana hao wa Madrid kushinda kombe hilo ambalo pia walilitwaa miaka 2010 na 2012.
Huzuni kubwa kwa Nahodha wa Marseille Dimitri Payet aliyeondoka uwanjani akichechemea kutokana na jeraha baada ya kukaa uwanjani nusu saa pekee, na sasa huenda akakosa kushiriki Kombe la Dunia kitun kilichomfanya Payet kudondosha chozi.
Bila kiungo huo wao, Wafaransa hao waliwatishia Atletico mara moja pekee, mshambuliaji wa zamani wa Fulham Kostas Mitroglou alipogonga mlingoti wa goli kwa mpira wa kichwa.
Share:

Wednesday, 16 May 2018

VIDEO : BODABODA WAONGELEA MAUAJI YA WENZAO BUKOBA

 Baadhi ya Madereva Pikipiki maarufu kama Bodaboda manispaa ya Bukoba mkoani Kagera wametoa kilio chao kwa serikali baada ya kuwepo kwa hali ya sintofahamu kufuatia kuuawa kinyama kwa madereva wenzao mfululizo ndani ya wiki moja.
Madereva wamesema kuwa wenzao wamepoteza maisha katika mazingira ya kutatanisha na wanauawa usiku wa manane pindi wanapopeleka abiria lakini cha kushangaza hawanyang’anyiwi kitu chochote wanakuta mwili wa marehemu pamoja na pikipiki pembeni.
SOURCE : MILLARD AYO.COM
Share:

MICHEZO : YANGA YAAMBULIA POINTI MOJA BAADA YA KUTOKA SARE NA RAYON SPORTS

Jumatano ya May 16 2018 uwanja wa Taifa Dar es Salaam Yanga walikuwa wenyeji wa Rayon Sports ya Rwanda kucheza mchezo wao wa pili wa Kundi D wa kombe la shirikisho Afrika CAF.

Yanga wakiwa nyumbani wameshindwa kuutumia vyema uwanja wa nyumbani baada ya kujikuta wanalazimishwa sare tasa (0-0) hivyo wanakuwa na point moja na wakishika mkia katika Kundi D ambalo linaongozwa na USM Alger ambayr ana point nne.


Mchezo mwingine wa kundi hilo ulikuwa kati ya USM Alger dhidi ya Gor Mahia waliyopo Kundi moja na Yanga, mchezo wao umemalizika kwa sare tasa pia hivyo Gor Mahia na Rayon Sports wote wanabaki kuwa na point mbili mbili kila mmoja, Yanga sasa atahitaji kuutumia vizuri mchezo wake wa tatu dhidi ya Gor Mahia kama atakuwa ameweka dhamira ya kweli ya kusonga mbele michuano ya CAF

MSIMAMO WA KUNDI BAADA YA MECHI ZA LEO

1. USM ALGERS      4 
2. GORMAHIYA        2
3.RAYON SPORTS   2
4. YOUNG AFRICANS 1

Share:

BURUDANI : WAZIRI MWAKYEMBE NAYE KAIONJA MOFAYA ENERGY DRINK YA ALIKIBA


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dr. Harrison Mwakyembe alikuwa ni mgeni rasmi katika uzinduzi wa urushwaji wa matangazo ya Kombe la Dunia kwa lugha ya kiswahili katika vituo vya TV1 na TBC,
Waziri Mwakyembe alikutana na Alikiba na akaonja kinywaji cha Mo Faya ambacho kinamilikiwa na Alikiba.
Share:

GUMZO : YULE MWIZI ALIYENASWA NA KIROBA CHA MAHINDI AACHIWA HURU

Mahakama ya Mwanzo Mlandizi mkoani Pwani imemuachia huru, kijana Frank Joseph (23) aliyeiba kiroba cha Mahindi debe 1 na kumnasia kichwani baada ya mlalamikaji kutofika mahakamani hapo mara 3 mfululizo.
Frank ambaye ni mkazi wa Mbezi DSM, ameachiwa huru na Hakimu Mfawidhi, Nabwike Mbaba wakati shauri hilo lilipoitishwa kwa ajili mlalamikaji (mtendewa) kutoa maelezo ya jinsi alivyoibiwa.

Hakimu Mbaba amesema kuwa kutokana na mlalamikaji (mtendewa) kushindwa kufika mahakamani hapo mara 3 mfululizo kutoa maelezo ya kuibiwa kwake anaifuta kesi huyo.
Share:

KIMATAIFA : NCHINI KENYA UKIPOST UJINGA KWENYE MTANDAO SASA FAINI NI MILLIONI MOJA

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametia saini mswada wa Sheria ya Uhalifu wa Kompyuta na Mtandaoni ya mwaka 2018 kuwa Sheria, hatua hii itatoa adhabu kali kwa watakaopatikana na makossa ya mtandaoni.
Sheria hiyo inatoa adhabu ya faini ya Milioni 100 (dola 50,000 za Marekani) au kifungo cha miaka miwili jela, au adhabu zote mbili, kwa atakayepatikana na kosa la uenezaji wa habari za uzushi.
Mtu atakayepatikana na kosa la kueneza taarifa ambazo zinaweza kuzua taharuki au kuzua vurugu atafungwa jela zaidi ya miaka kumi.
Share:

MICHEZO : MAGUFULI AKUBALI KUWAKABIDHI KOMBE MABINGWA SIMBA JUMAPILI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Joseph Magufuli amekubali kuwakabidhi Kombe la ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Simba SC Jumamosi Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
Hayo yamesemwa mchana wa leo na Mtendaji Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wilfred Kidau alipozungumza na Waandishi wa Habari leo makao makuu ya ofisi za shirikisho, Uwanja wa Karume, Ilala mjini Dar es Salaam.
.

Kidau amesema Rais Magufuli kabla ya kuwakabidhi Simba SC Kombe la ubingwa wa Ligi Kuu, ataanza kwa kukabidhiwa Kombe la ubingwa wa michuano ya Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 (CECAFA U17), ambalo Tanzania ilitwaa mapema mwezi huu nchini Burundi. 
Share:

Sunday, 13 May 2018

NGORONGORO HEROES YAAMBULIA KIPIGO BIFU LA KOCHA NA MCHEZAJI MAUMIVU KWA TAIFA

TANZANIA imejiweka kwenye mazingira magumu ya kusonga mbele katika mchujo wa kuwania tiketi ya Fainali za Vijana chini ya umri wa miaka 20 Afrika, baada ya kufungwa mabao 2-1 na Mali jioni ya leo Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
Tanzania, Ngorongoro Heroes sasa watalazimika kwenda kushinda ugenini kuanzia 2-0 Mei 20 mjini Bamako katika mchezo wa marudiano ili kuingia hatua ya mwisho ya mchujo wa kuwania tiketi ya Niger mwakani.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na marefa kutoka Comoro, Soulaimane Ansudane aliyepuliza kipyenga akisaidiwa na washika vibendera Mmadi Faissoil na Abdoulmadjid Azilani, hadi mapumziko tayari Mali walikuwa mbele kwa mabao 2-1.
Ousmane Diakite alianza kuifungia Mali dakika ya 37 akitumia makosa ya kipa wa Ngorongoro Heroes, Abdultwali Msheri kupiga mpira bila uangalifu, ambao ulinaswa na wapinzani na kufunga.
Wakati Ngorongoro Heroes wanahangaika kutafuta bao la kusawazisha, wakajikuta wakichapwa bao la pili rahisi kwa makosa ya kipa tena, mfungaji Samadiare Dianka kwa shuti la mpira wa adhabu.
Msheri alikwenda kusimama nyuma ya ukuta wa wachezaji wake na kumrahisishia Dianka kazi kwa kuupeleka mpira upande uliokuwa wazi, kushoto kwa mlinda mlango huyo.
Mshambuliaji chipukizi wa Azam FC, Paul Peter akaifungia Ngorongoro Heroes bao la kufutia machozi dakika ya 44 akiuwahi mpira uliotemwa na kipa wa Mali, Youssouf Keita kufuatia shuri la mpira wa adhabu.
Kipindi cha pili mvua iliyoanza kunyesha tangu asubuhi ikaongezeka na ladha ya mpira ikapungua kutokana na uwanja kuwa unateleza na haikuwa ajabu matokeo hayakubadilika.
Kipigo cha leo lawama zinakwenda kwa Kocha Mkuu, Ammy Ninje ambaye  hakumpanga kipa namba moja, Ramadhani Kabwili ambaye alitofautiana naye kabla ya mchezo wa leo.
Share:

YANGA HALI TETE YAPIGWA NA MTIBWA SUGAR 1-0

YANGA SC leo imecheza mechi ya saba bila ushindi, baada ya kuchapwa 1-0 na Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
Na bao lililoizamisha Yanga SC leo limefungwa na mchezaji wao wenyewe wa zamani, kiungo Hassan Dilunga dakika ya 82.
Kipigo hicho kinazidi kuwaweka Yanga katika mazingira magumu ya kumaliza Ligi Kuu ndani ya nafasi tatu za juu, kwani sasa wakiwa wamecheza mechi 26 wanazidiwa pointi nne na Azam FC walio nafasi ya pili kwa pointi zao 52 za mechi 28.

Mara ya mwisho Yanga kushinda ilikuwa ni Aprili 7, mwaka huu walipoichapa 2-0 Welayta Dicha ya Ethiopia katika mchezo wa kwanza wa mchujo wa kuwania kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika wakiwa chini ya kocha wao, Mzambia George Lwandamina.
Baada ya mchezo huo, Lwandamina alipakia mizigo yake kurejea kwao na tangu hapo Yanga hawajashinda tena, katika mechi saba, wakifungwa tano na kutoa sare mbili.
Baada ya mchezo wa leo, Yanga SC inarejea Dar es Salaam kwa ajili ya mchezo wake wa Jumatano wa Kundi D Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Rayon Sport ya Rwanda Uwanja wa Taifa.
Mechi nyingine ya Ligi Kuu leo, Mbeya City imelazimishwa sare ya 0-0 na Tanzania Prisons katika mechi ya mahasimu wa Jiji la Mbeya Uwanja wa Sokoine.
Share:

USHAURI WA KOCHA ZAHERA KWA YANGA

KOCHA mpya mtarajiwa wa Yanga SC, Mwinyi Zahera kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ameshauri uongozi kupeleka kikosi cha timu ya vijana, maarufu kama Yanga B katika mechi zake mbili za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhid ya Tanzania Prisons mjini Mbeya na Mtibwa Sugar mjini Morogoro, ili kikosi cha kwanza kiendelee na maandalizi ya mchezo ujao wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Rayon Sport ya Rwanda Jumatano ijayo.
Zahera amesema kwa sasa Yanga wanapaswa kuelekeza nguvu zao kwenye mechi za Kombe la Shirikisho la Soka Afrika baada ya kupoteza nafasi ya kutetea ubingwa wa Ligi Kuu.
Zahera ameyasema hayo leo mchana Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam wakati kikosi cha Yanga kikiwasili kutoka Algiers nchini Angeria ambako Jumapili kilifungwa mabao 4-0 na wenyeji, U.S.M. Alger katika mchezo wake wa kwanza wa Kundi D Kombe la Shirikisho Uwanja wa Julai 5, 1962.

“hatuna nafasi kwenye ligi, hivyo tunatakiwa kuweka nguvu zote kwenye kombe la Shirikisho, nimewaomba viongozi wapeleke kikosi B katika michezo yetu ya ligi, ili nibaki na kikosi cha kwanzaa nikiandae kwa ajii ya mchezo dhidi ya Rayon,”. 
"Tunatakiwa kujiandaa vema ili tusipoteze mchezo huo, ukiangalia ratiba ya ligi imekaa vibaya kwetu,  tumefika leo, kesho tunatakiwa kwenda Mbeya, baadaye tuna mchezo Morogoro, kabla ya kuivaa Rayon,  ndio maana nimewaomba wakubwa tuwaze zaidi kombe la Shirikisho,”amesema.
Share:
Powered by Blogger.

IDADI YA WANAOTEMBELEA BLOG HII

Blog Archive

Recent Posts

Fashion

3/Fashion/big-col-right

Recent Posts

Header Ads

Followers

Powered By Blogger

Tags

Maoni

3/recent-comments

WASILIANA NASI

Popular Posts

Labels

Blog Archive

Blogger templates