Kikosi cha mabingwa wa Tanzania bara Azam fc kinondoka nchini hapo leo usiku kwa kutumia shirika la ndege ya Ethiopia, kuelekea Sudan kwa ajili ya mchezo wa marejeano wa klabu bingwa Afrika utakao chezwa siku ya jumamosi usiku.
Kwa mujibu wa kauli ya meneja wa Azam FC Jemedari Said amesema kuwa msafara huo utakuwa na wachezaji 21 pamoja na viongozi 8.
Azam fc wanahitaji sare ya aina yoyote ile ili iingie katika hatua ya kwanza ya michuano hiyo, ikiwa ni baada ya kuibuka na ushindi wa goli 2-0 katika uwanja wa azam complex
Kikosi cha Yanga kinatarajia kuondoka nchini kesho kwenda Botswana kwa ajili ya kuwavaa BDF XI katika mechi ya Kombe la Shirikisho.
Yanga itaondoka nchini ikiwa na kikosi cha wachezaji 20 pamoja na memba wa benchi la ufundi pamoja na baadhi ya viongozi.
Katika mechi ya kwanza, Yanga ikiwa nyumbani ilishinda kwa mabao 2-0 yaliyofungwa na Mrundi, Amissi Tambwe.
Safari hiyo ya Yanga kwenda Botswana ni kumalizia mechi hiyo ya pili.
Kabla ya safari hiyo, Yanga ikiongozwa na Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm ilishinda mechi tatu ikianza kwa kuitwanga BDF XI kabla ya kuhamia kwenye ligi.
Katika mechi za Ligi Kuu Bara, Yanga ilianza kwa kuifunga
Prisons kwa mabao 2-0, halafu ikageuka na kuichapa Mbeya City kwa mabao 3-1 kuthibitisha kuwa haikubahatisha
0 comments:
Post a Comment