Pages

Tuesday, 24 February 2015

UEFA BARCELONA YAPATA USHINDI 2-1 DHIDI YA MAN CITY SUAREZ SHUJAA ATUPIA ZOTE NAO JUVE WAPATA USHINDI 2-1 DHIDI YA DORTMUND

Bao 2 za Luis Suarez, akicheza Mechi yake ya kwanza Nchini England tangu aihame Liverpool mwanzoni mwa Msimu, zimewapa Barcelona ushindi wa Bao 2-1 walipocheza na Manchester City waliokuwa kwao Etihad katika Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA CHAMPIONZ LIGI.
Bao hizo za Suarez zilifungwa Dakika za 16 na 30 lakini Sergio Suarez akaipa City matumaini kwenye Mechi hiyo baada ya kufunga Bao katika Dakika ya 69

Matumaini hayo ya City kwenye Mechi hiyo yalizimwa katika Dakika ya 74 baada ya Beki wao Gael Clichy kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu kufuatia Kadi za Njano 2 na hili limeendeleza mtindo wa City kumaliza Mechi na Barca wakiwa Mtu 10 kama ilivyokuwa Msimu uliopita kwenye Mechi zote za Raundi hii walizofungwa na Barca Mchezaji wao mmoja alipata Kadi Nyekundu.
Katika Dakika ya 90 Barca walipewa Penati pale Beki wao Pablo Zabaleta alipomchezea Rafu Lionel Messi lakini Penati hiyo iliyopigwa na Messi iliokolewa na Kipa Joe Hart na Mpira kumrudia tena Messi aliepiga Kichwa nje.
Timu hizi zitarudiana Nou Camp hapo Machi 18.
MECHI NYINGINE JANA
Juventus FC 2 BV Borussia Dortmund 1
Juventus wakicheza kwao Juventus Arena wameichapa Borussia Dortmund Bao 2-1 katika Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA CHAMPIONZ LIGI.
Bao za Juve zilifungwa na Carlos Tevez, Dakika ya 13, na Alvaro Morata, Dakika ya 42, huku Dortmund wakifunga Bao lao kupitia Marco Reus katika Dakika ya 18.

Timu hizi zitarudiana huko Signal Iduna Park, Nyumbani kwa Dortmund, hapo Machi 18.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

IDADI YA WANAOTEMBELEA BLOG HII

Blog Archive

Recent Posts

Fashion

3/Fashion/big-col-right

Recent Posts

Header Ads

Followers

Powered By Blogger

Tags

Maoni

3/recent-comments

WASILIANA NASI

Popular Posts

Labels

Blog Archive

Blogger templates