FA, Chama cha Soka England, kimempunguzia Adhabu Kiungo wa Chelsea Nemanja Matic kutoka Mechi 3 na kuwa 2 lakini ataikosa Fainali ya Capital One Cup hapo Jumapili dhidi ya Tottenham.
Adhabu hiyo imepunguzwa kufuatia Chelsea kukata Rufaa kupinga Kadi Nyekundu aliyopewa Jumamosi wakati Chelsea wanatoka Sare 1-1 na Burnley kwenye Mechi ya Ligi Kuu England Uwanjani Stamford Bridge.
Matic, Kiungo wa Miaka 26 kutoka Serbia, alitolewa nje kwa Kadi Nyekundu katika Dakika ya 70 alipomsukuma na kumwangusha Ashley Barnes ambae alimchezea Rafu mbaya.
Licha ya kupunguziwa Adhabu, Chelsea wamepokea uamuzi huo kwa masikitiko na kuhuzunika na sasa wanangojea Taarifa rasmi ya FA ili kutoa tamko lao rasmi.
Mbali ya kuikosa hiyo Fainali ya Jumapili dhidi ya Tottenham, Matic pia ataikosa Mechi ya Ligi ya Jumatano Machi Ugenini huko Upton Park dhidi ya West Ham.
0 comments:
Post a Comment