Pages

Wednesday, 25 February 2015

BAADA YA KUSIMAMISHWA KWA LIGI YA MISRI SASA LIGI HIYO KUANZA TENA MWEZI UJAO BILA MASHABIKI

LIGI Kuu ya Misri ambayo ilisimamishwa, itaendelea tena mwezi ujao lakini bila ya kuruhusiwa mashabiki kuishuhudia michezo hiyo kutokana na kukithiri kwa matukio ya vurugu yaliyoleta maafa ya mashabiki hivi karibuni.
Ligi hiyo ilisimamishwa baada ya kutokea vurugu uwanjani na kuua watu karibu 19 kutokana na vurugu hizo za mashabiki na polisi nje ya uwanja jijini hapa Februari 8 mwaka huu.
Baada ya kikao cha Jumatano, Baraza la Mawaziri la Misri katika taarifa yake lilisema kuwa, ligi inaweza kuendelea "bila ya mashabiki baada ya kumalizika kwa siku 40 za maombolezo ".
Hata hivyo, taarifa hiyo haikusema bayana ni lini hasa ligi hiyo itaanza kuchezwa huku mashabiki wakizuiwa kushuhudia mechi hizo.
Maafa hayo yalitokea kabla ya mchezo kati ya klabu za jijini Cairo ya Zamalek na ENPPI wakati polisi na mashabiki walipopambana.
Polisi walilipua mabomu ya machozi na kurusha silaha nyingine kwa mashabiki hao, ambao walikuwa wakilazimisha kuingia uwanjani kushuhudia pambano hilo.
Hiyo ilikuwa ni mara ya kwanza kwa idadi maalum ya mashabiki kuruhusiwa kuingia uwanjani kushuhudia mechi za ligi tangu Februari 2012, wakati mashabiki 72 wa Al Ahly walipokufa walipokuwa wakipambana na wenzao wa Al Masry kwenye uwanja wa Port Said.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

IDADI YA WANAOTEMBELEA BLOG HII

Blog Archive

Recent Posts

Fashion

3/Fashion/big-col-right

Recent Posts

Header Ads

Followers

Powered By Blogger

Tags

Maoni

3/recent-comments

WASILIANA NASI

Popular Posts

Labels

Blog Archive

Blogger templates