Borussia Dortmund wameendelea kujinusuru kwenye Bundesliga baada ya kuwa na wasiwasi wa kushushwa Daraja na kuelendelea kupanda juu kwenye Msimamo wa Ligi hiyo ya Ujerumani baada ya Jana kuifunga Ugenini Bao 3-2 Stuttgart.
Mchezaji wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang ndie aliwafungia Bao la kwanza kufuatia Pasi ya Shinji Kagawa lakini Stuttgart wakasawazisha kwa Bao la Penati la Florian Klein iliyotolewa kufuatia Nuri Sahin kumwangusha Georg Niedermeier.
Dortmund walikwenda mbele Bao 3-1 kwa Bao za Ilkay Gundogan na Marco Reus lakini Sttugart walikomboa Bao moja katika Dakika za mwishoni.
0 comments:
Post a Comment