Pages

Friday, 20 February 2015

LIGI KUU UINGEREZA LEO MECHI 7 DIMBANI VIGOGO WOTE KUSAKA POINTI NYUMBANI NA UGENINI

LIGI KUU ENGLAND Leo inarudi tena dimbani baada ya kukosekana Wikiendi iliyopita kwa kupisha FA CUP kwa Mechi 7 ambazo pia zitawahusisha Vinara Chelsea na Vigogo wengine wakiwemo Mabingwa Watetezi Manchester City, Man United na Arsenal.
Mechi 6 zitachezwa Saa 12 Jioni hii Leo na Man City kumalizia kwa Mechi ya mwisho wakiwa Nyumbani kuivaa Newcastle.
Vinara Chelsea, wanaoongoza Ligi wakiwa Pointi 7 mbele ya Man City, wako kwao Stamford Bridge kucheza na Burnley wakati Timu ya Tatu Man United wako Ugenini Liberty Stadium kucheza na Swansea City ambayo iliifunga Man United Bao 2-1 Uwanjani Old Trafford katika Siku ya ufunguzi wa Ligi Mwezi Agosti ikiwa ni Mechi ya kwanza kabisa ya Ligi kwa Meneja Louis van Gaal.
Lakini safari hii Man United wako ngangari kidogo baada ya kufungwa Mechi 1 tu katika Mechi 19 ukilinganisha na Swansea ambao wameshinda Mechi 1 tu kati ya 7 za Ligi walizocheza mwisho na pia kupigwa na kutupwa nje ya FA CUP na Blackburn Rovers.
Mechi nyingine hii Leo ni Arsenal kuwa Ugenini huko Selhurst Park, Croydon, Kitongoji cha Jiji la London kuivaa Crystal Palace.
Hivi sasa Arsenal wako Nafasi ya 5 wakiwa Pointi 1 nyuma ya Tmu ya 4 Southampton ambao wako dimbani Kesho wakiwa kwao kucheza na Liverpool.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

IDADI YA WANAOTEMBELEA BLOG HII

Blog Archive

Recent Posts

Fashion

3/Fashion/big-col-right

Recent Posts

Header Ads

Followers

Powered By Blogger

Tags

Maoni

3/recent-comments

WASILIANA NASI

Popular Posts

Labels

Blog Archive

Blogger templates