Pages

Friday, 20 February 2015

LA LIGA MECHI NNE LEO NAFASI KWA BARCLONA KUKAMATA USUKANI WA LIGI YA HISPANIA

BARCELONA Leo wana nafasi safi sana kuiporomosha Real Madrid kutoka kilele cha La Liga wakati watakapocheza kwao Nou Camp na Malaga.
Real ndio Vinara wa La Liga wakiwa Pointi 1 mbele ya Barcelona lakini wao hawapo Uwanjani hadi Kesho watakapocheza Ugenini na Elche na hivyo hii ni nafasi murua kwa Barca kuwa Vinara wapya.
Pengine hii ni kazi laini kwa Barca ambao Fowadi yao ya Mtu 3 hatari ya Lionel Messi, Luis Suarez na Neymar sasa imeanza kuwa moto.
Hii Leo pia, Mabingwa Watetezi Atletico Madrid, ambao walichapwa 2-0 na Celta Vigo katika Mechi iliyopita na kubaki wakiwa Nafasi ya 3 Pointi 6 nyuma ya Barca, wapo Nyumbani kwao Vicente Calderon kucheza na UD Almeria.
Mechi nyingine hii Leo ni kati ya Cordoba CF na Valencia CF na kumalizia Mechi kati ya Deportivo La Coruna na Celta de Vigo.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

IDADI YA WANAOTEMBELEA BLOG HII

Blog Archive

Recent Posts

Fashion

3/Fashion/big-col-right

Recent Posts

Header Ads

Followers

Powered By Blogger

Tags

Maoni

3/recent-comments

WASILIANA NASI

Popular Posts

Labels

Blog Archive

Blogger templates