Msanii hip hop, Rashid Makwiro 'Chid Benz' amehukumiwa miaka miwili kwenda jela.
Hukumu
hiyo imetolewa leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Kisutu jijini Dar
es Salaam ambako kesi yake ya kukamatwa na madawa ya kulevya ilikuwa
inasikilizwa.
Hukumu
ilikuwa ni adhabu ya miaka miwili jela au kulipa faini ya Sh 9,000,000
ambayo aliilipa baada ya watu wake kujitokeza na kukamilisha hilo na
sasa Chid Benz.
Kesi
yake hiyo iliyoendeshwa kwa wiki kadhaa, ilitokana na msanii huyo
kukamatwa na madawa ya kulevya kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere
akiwa njiani kwenda mjini Mbeya kwa ajili ya shoo.
Chid Benz alikiri madawa aliyokamatwa nayo kwenye mfuko wa shati yalikuwa yake.
0 comments:
Post a Comment