Yanga imekuwa klabu ya kwanza nchini Tanzania kulipa posho za wachezaji vizuri kuliko timu yoyote Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Awali Yanga ilikuwa ikiwapa posho wachezaji wake sh 70,000 kwa mechi wanazoshinda kwa wale wanaoingia Uwanjani na 35,000 kwa wale ambao hawakupangwa.
Kupitia kwa Mwenyekiti wake, Yusuf Manji timu hiyo imefanya kufuru ambapo sasa kila mechi watakayoshinda wachezaji 18 watapata posho ya Sh 140,000 huku wale ambao hawakuvaa jezi watapata sh 98,000.
Kwa maana hiyo Yanga itakuwa inawalipa wachezaji wake vizuri kuliko mtani wake wa jadi Simba na klabu tajiri ya Azam FC.
Awali timu ya Azam FC ndio ilikuwa inalipa vizuri ikiwa inalipa sh. 130,000 kwa mechi wanazoshinda. Huku Simba wakilipa sh, 50,000.
0 comments:
Post a Comment