Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Wanawake Tanzania (Twiga Stars),
Rogasian Kaijage ametangaza kikosi cha wachezaji thelathini, kitakachoingia
kambini siku ya Jumapili kujiandaa na mchezo wa kufuzu Mataifa Afrika dhidi ya
Zambia mwezi Machi mwaka huu.
Kaijage ametangaza program yake ya mazoezi
itakayochukua takribani wiki nne (4) ili kuhakikisha wachezaji wanakua tayari
kwa ajili ya mchezo huo utakaochezwa kati ya Machi 21, 22 mwaka huu, huku
akipanga kucheza mchezo mmoja wa kirafiki kabla ya kuelekea Lusaka Zambia
kwenye mchezo wa awali.
0 comments:
Post a Comment