Pages

Saturday, 21 February 2015

LIGI KUU UINGEREZA MAN CITY SHUJAA YASHINDA 5-0, ARSENAL NAO USHINDI MAN UNITED KIPIGO, CHELSEA SARE

Mabingwa Manchester City Jana wamapata ushindi wao mkubwa Msimu huu kwenye Ligi Kuu England walipoitandika Newcastle Mabao 5-0 Uwanjani Etihad na kujizatiti kwenye Nafasi ya Pili wakilikata pengo na Vinara Chelsea kuwa Pointi 5 baada ya Vinara hao kutoka Sare 1-1 na Burnley hapo Jana.
City, wakicheza tena na Kiungo wao mahiri Yaya Toure aliekuwa na Timu yake ya Taifa Ivory Coast Mwezi Januari na mwanzoni mwa Februari pamoja na Mchezaji mpya Wilfried Bony alieanzia Benchi hapo Jana walitawala Mechi hii.
City walitangulia kupata Bao kwa Penati ya Dakika ya Pili tu kufuatia makosa ya Anita kuupoteza Mpira na kumchezea Rafu Edin Dzeko na Penati hiyo kufungwa na Sergio Aguero.
Dakika 10 baadae Samir Nasri alipiga Bao la Pili na Dakika ya 21 Edin Dzeko kutia Bao la 3.
Kipindi cha Pili David Silva aliongeza Bao 2 katika Dakika za 51 na 53.
Crystal Palace 1 Arsenal 2
Penati ya Santi Cazorla na Bao la Olivier Giroud
, yote Kipindi cha Kwanza, yamewapa Arsenal wa Ugenini wa Bao 2-1 walipoichapa Crystal Palace na kutwaa Nafasi ya 3 kwa kuishusha Man United Nafasi ya 4.
Bao pekee la Palace lilifungwa Dakika ya 90 na GlennMurray.
Chelsea 1 Burnley 1
Chelsea, wakichezwa kwao Stamford Bridge, wametoka Sare 1-1 na Burnley ambayo inapigana isishushwe Daraja.
Chelsea walitangulia kufunga kwa Bao la Branislav Ivanovic la Dakika ya 14 lakini wakawa pungufu katika Dakika ya 70 pale Nemanja Matic alipopewa Kadi Nyekundu alipolipizia Rafu toka kwa Ashley Barnes.
Burnley walisawazisha kwa Bao la Kichwa la Ben Mee kufuatia Kona ya Dakika ya 81.
Swansea 2 Manchester United 1
Kama walivyofanya katika Mechi ya ufunguzi wa Msimu huu huko Old Trafford Mwezi Agosti, Swansea Leo hii wakiwa kwao Liberty Stadium wameipiga Man United Bao 2-1.
Man United walitangulia kufunga kwa Bao la Anders Herrera la Dakika ya 28 na Swansea kusawazisha Dakika ya 30 kwa Bao la Ki Sung-yueng na kisha Gomis kuwapa ushindi kwa bao la kibahati baada ya Shuti la Mita 25 la Jonjo Shelvey kumbabatiza usoni na kumhadaa Kipa David de Gea.   
Share:

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

IDADI YA WANAOTEMBELEA BLOG HII

Blog Archive

Recent Posts

Fashion

3/Fashion/big-col-right

Recent Posts

Header Ads

Followers

Powered By Blogger

Tags

Maoni

3/recent-comments

WASILIANA NASI

Popular Posts

Labels

Blog Archive

Blogger templates