Hii Leo wakicheza nyumbani Ndanda FC wameutumia vyema uwanja wao
wa nyumbani Nangwanda baada ya kuitandika Coastal Union ya tanga goli 1-0
katika mchezo ulioonekana kuwa mgumu kwani hadi mapumziko kila timu haikuona
labgo la mwenzie
Goli pekee la ndanda limefungwa kipindi cha pili dk ya 73
Kagera Sugar wakiwa
Kambarage Mjini Shinyanga wamepata ushindi wa goli moja dhidi ya Polisi Moro wakati
Mgambo JKT wakiwa Mkwakwani Mjini Tanga wameitandika Mtibwa Sugar goli 1-0
Jumapili
ndiyo Siku ya Vigogo wakati Yanga, ambao wanaongoza Ligi wakiwa Pointi 2 mbele
ya Mabingwa Watetezi Azam FC, wako huko Sokoine Mjini Mbeya kucheza na Watoto
wa Nyumbani, Mbeya City.
Pia
Jumapili Simba wako Ugenini huko Shinyanga kucheza na Stand United na Azam FC
wako kwao Azam Complex, Chamazi kwenye Viunga vya Jiji la Dar es Salaam kucheza
na Tanzania Prisons.
0 comments:
Post a Comment