Floyd Mayweather Junior
atazichapa na Manny Pacquiao jijini Las Vegas
nchini Marekani Mei 2.

Mmarekani Mayweather, 37, na Mfilipino Pacquiao, 36, wanaaminika ndiyo mabondia bora zaidi wa kizazi hiki kwa uzito wao.
Mayweather ni bingwa wa WBC na WBA kwa welterweight na Pacquiao anashikilia ubingwa wa WBO.
Mayweather hajawahi kupigwa katika mapambano yake yote 47 ya ngumi za kulipwa wakati Pacquiao ameshinda mapambano 57 ikiwa ni kumi zaidi ya Mayweather, lakini amepoteza matano katika yote 64 aliyocheza.
Pambano hilo kwa ujumla
linatarajiwa kugharimu pauni milioni 162m au dola milioni 250.
0 comments:
Post a Comment