Uongozi wa Stand united umeamua kuwanyang'anya simu wachezaji wake ili kuhakikisha hakuna hujuma kabla ya kuwavaa Simba kesho kwenye Uwanja wa
Kambarage mjini Shinyanga.
Habari za ndani kutoka
Stand United zinaeleza kila mchezaji amekabidhi simu yake kwa uongozi.
“Wachezaji wametakiwa
kukabidhi simu kwa uongozi na hilo limefanyika kwa ajili ya uhakika tu.
“Si kwamba Simba
wametuhujumu, lakini kwa kuwa ni timu kubwa lazima tuwe makini sana katika
hili,” kilieleza chanzo.
Stand itakuwa na kazi ya
kuizuia Simba kesho ili angalau kukusanya pointi zitakazoikwamua eneo la
mkiani.
Tayari Simba iko mjini
Shinyanga tayari kwa mechi hiyo inayotarajiwa kuingiza idadi kubwa ya watu.
0 comments:
Post a Comment