Pages

Friday, 6 March 2015

ANGALIA KIKOSI CHA BRAZIL KITAKACHOCHEZA NA CHILE MWEZI HUU COUTHINO,ROBHINO NA MARCELO WARUDISHWA KIKOSINI

WINGA wa Liverpool Philippe Coutinho ni mmoja wa Wachezaji Watano wanaochezea Klabu za England waliotajwa kwenye Kikosi cha Timu ya Taifa ya Brazil na Kocha Dunga ambacho kitacheza Mechi za Kirafiki baadae Mwezi huu na France na Chile.
Coutinho aliichezea Brazil kwa mara ya kwanza Mwaka 2010 lakini baada ya hapo hakuitwa tena hadi Mwaka Jana baada ya Kombe la Dunia walipoadhiriwa kwao baada ya kufumuliwa Bao 7-1 na Germany kwenye Nusu Fainali.
Msimu huu Coutinho, mwenye Miaka 22, yuko moto na Wikiendi iliyopita ndie aliefunga Bao la ushindi murua wakati Klabu yake Liverpool inawachapa Mabingwa wa England Man City Bao 2-1 Uwanjani Anfield.
Wachezaji wengine wanaocheza Ligi Kuu England ambao wameitwa na Kocha Dunga ni Kiungo wa Man City Fernandinho pamoja na Wachezaji Watatu wa Chelsea Oscar, Willian na Filipe Luis.
Wachezaji waliorudishwa tena Kikosini ni Robinho, anaechezea Santos huko Brazil, na Marcelo wa Real Madrid.
Brazil itacheza na France ndani ya Stade de France Mjini Paris hapo Machi 26 na Machi 29 kucheza na Chile kwenye Uwanja wa Arsenal, Emirates Stadium, Jijini London.
KIKOSI KAMILI:
Makipa: Jefferson, Diego Alves, Marcelo Groeh
Mabeki: David Luiz, Marquinhos, Thiago Silva, Miranda, Filipe Lui­s, Danilo, Fabinho, Marcelo.
Viungo: Luiz Gustavo, Fernandinho, Elias, Souza, Oscar, Willian, Douglas Costa, Philippe Coutinho.
Mafowadi: Neymar, Robinho, Roberto Firmino, Diego Tardelli.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

IDADI YA WANAOTEMBELEA BLOG HII

Blog Archive

Recent Posts

Fashion

3/Fashion/big-col-right

Recent Posts

Header Ads

Followers

Powered By Blogger

Tags

Maoni

3/recent-comments

WASILIANA NASI

Popular Posts

Labels

Blog Archive

Blogger templates