YANGA imeiacha mbali Platinum ya Zimbabwe katika ulipaji wa mishahara kwani mchezaji anayelipwa zaidi kwenye timu hiyo watakayokutana nayo kwenye raundi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho anachukua Dola 1,000 (Sh1.8 milioni) wakati anayelipwa zaidi Yanga anachukua Dola 3,000 (Sh5.4 milioni).
Taarifa za ndani ya Platinum ambazo Mwanaspoti inazo ni kwamba Platinum ndiyo timu inayoongoza Zimbabwe kwa kuwalipa vizuri wachezaji wake kwa kuwapatia posho ya Dola 400 (Sh720,000) kwa kila mchezaji kwa michezo wanayoshinda huku mchezaji anayelipwa ghali akichukua dola 1,000 (Sh 1.8milioni) ni theluthi moja ya Emmanuel Okwi wa Simba anayelamba Dola 3,000 sawa na straika Mliberia wa Yanga, Kpah Sherman.
SOURCE: MWANA SPOTI
Sunday, 8 March 2015
Home »
» ANGALIA MISHAHARA YA WACHEZAJI WA PLATINUM FC ITAKAYOCHEZA NA YANGA MCHEZO WA KOMBE LA SHIRIKISHO HAWAIFIKII HATA KIDOGO
0 comments:
Post a Comment