JANA huko Anfield, Liverpool walibanwa na Timu ya Daraja la chini la Championship Blackburn Rovers na kutoka Sare ya 0-0 katika Robo Fainali ya FA CUP.
Timu hizi sasa zitalazimika kurudiana huko Ewood Park Nyumbani kwa Blackburn Rovers ambayo tayari ambayo iliziswaga Timu nyingine za Ligi Kuu England, Swansea City na Stoke City, na kutinga hii Robo Fainali.
Kwenye Mechi ya Jana, Liverpool walianza vibaya baada ya Sentahafu wao Martin Skrtel kuanguka vibaya na kuumia Kichwani na kusababisha Mechi kusimama kwa Dakika 8 hadi anatolewa nje kwa Machela.
Tayari zimeshachezwa Robo Fainali 3 na mbili zimetoa Sare wakati ni Aston Villa pekee ndie aleshinda na kutinga Nusu Fainali.
Leo Robo Fainali zitamalizika huko Old Trafford wakati Man United watakapocheza na Mabingwa Watetezi Arsenal.
Leo Jumatatu Usiku Arsenal watakuwa Old Trafford kutetea Taji lao la FA CUP kwenye Mechi ya Robo Fainali dhidi ya Manchester United, Meneja wao Arsène Wenger akisema kuwa Bao la Ryan Giggs bado linamwandama akilini.
Bao hilo la Giggs alilifunga katika Marudiano ya Nusu Fainali ya FA CUP ya Mwaka 1999 iliyochezwa Uwanjani Villa Park na Mechi hiyo imeingizwa kwenye Historia kama Mechi ya kukumbukwa.
Mechi hiyo iliipeleka Man United kuandika Historia ya kutwaa Trebo, yaani Ubingwa wa Ligi Kuu England, FA CUP na UEFA CHAMPIONZ LIGI katika Msimu mmoja.
Ingawa Arsenal imeshafungwa mara 3 kwenye FA CUP tangu wakati huo, Arsenal imeifunga mara mbili Man United kwenye FA CUP ikiwani pamoja na ile Fainali ya Mwaka 2005.
0 comments:
Post a Comment