Mshambuliaji wa kimataifa Emmanuel Okwi, Leo hii amerudisha furaha ya mashabiki wa Simba baada ya kufunga Bao pekee na la ushindi walipoilaza Yanga Bao 1-0 kwenye Mechi ya Ligi Kuu Vodacom.
Bao hilo la Okwi lilifungwa Dakika ya 53 na kuipandisha Simba hadi Nafasi ya 3 wakiwa na Pointi 26 kwa Mechi 17 na juu yao wapo Mabingwa Watetezi Azam FC wenye Pointi 30 kwa Mechi 16 na Yanga bado wapo kileleni wakiwa na Pointi 31 kwa Mechi 16.
Yanga walimaliza Mechi hii wakibaki Mtu 10 baada ya Mchezaji wao Haruna Niyonzima kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu karibuni na mwisho.
Yanga na Simba zimekutana mara 103, kati ya hizo, Yanga ilishinda 38, Simba 32,huku mara 33 zikitoka sare.
Nao ndanda wakicheza ugenini jijini tanga wamekubali kipigo cha magoli 3 kwa 1 kutoka mgambo Jkt magoli ya mgambo yamefungwa na Salim Aziz Gilla aliyefunga magoli mawili dakika ya 12na 70 huku lingine likifungwa na Malimi Busungu dk 26 goli pekee la Ndanda Gideon Benson dk 45
Huko Manungu Mtibwa sugar wametoka sare ya goli 1-1 dhidi ya Mbeya city goli la Mtibwa limefungwa kwa kichwa dk 14 na Musa hasani mgosi akiunganisha mpira wa adhabu uliopigwa na na goli la mbeya city limefungwa na themi felix
0 comments:
Post a Comment