Jose Mourinho ameelezea nia yake kutwaa Mataji mengine mara baada ya Jana Uwanjani Wembley Jijini London Timu yake Chelsea kuichapa Tottenham Hotspur Bao 2-0 na kubeba Capital One Cup likiwa ni Kombe lake la kwanza tangu arejee kwa mara ya pili Klabuni Chelsea.Ushindi huo unakuja baada ya ukame wa siku 914 bila Chelsea kuwa na taji

Bao za Chelsea hapo Jana zilifungwa na Nahodha John Terry na Kyle Walker aliejifunga mwenyewe.
Akiongea mara baada ya Mechi hiyo, Jose Mourinho alisema: “Mie ni kama mtoto alieshinda mara ya kwanza. Ni ngumu kwangu kuishi bila Mataji. Nahitaji kutwaa Makombe!”
Mourinho, ambae alikuwa Chelsea kwa mara ya kwanza kati ya Miaka 2004 na 2007 na kurejea 2013, sasa ameshatwaa Vikombe 7 akiwa na Chelsea.
0 comments:
Post a Comment