Pages

Sunday, 1 March 2015

LA LIGA- REAL MADRID WACHEMKA WATOA SARE NA VILLAREAL NYUMBANI, ATLETICO NAO SARE

VINARA wa La Liga Real Madrid Jana Usiku wakiwa kwao Santiago Bernabeu walishindwa kupanua pengo lao na Timu ya Pili Barcelona baada ya kutoka Sare ya 1-1 na Villareal.
Huku wakikabiliwa na Mechi ya Nusu Fainali ya Kombe la Mfalme hapo Jumatano dhidi ya Barcelona, Kocha wa Villareal Marcelino aliamua kuchezesha Kikosi dhaifu lakini kilipigana na kuwasimamisha Real kwao.
Real walipata Bao lao kwa Penati ya Dakika 52 iliyofungwa na Cristiano Ronaldo baada ya yeye mwenyewe kuvutwa na kuangushwa na Eric Bailly.
Gerard Moreno katika Dakika ya 64 aliisawazishia Villareal kwa Shuti la chini ambalo Kipa Iker Casillas alishindwa kulizuia.
Real bado wapo kileleni wakiwa na Pointi 61 wakifuatiwa na Barca wenye Pointi 59 na Mabingwa Watetezi Atletico Madrid wakiwa na Pointi 54.
MATOKEO YA MECHI NYINGINE
Valencia C.F 2 Real Sociedad 0    
SD Eibar 0 Athletic de Bilbao 1   
Sevilla FC 0 Atletico de Madrid 0 
Real Madrid CF 1 Villarreal CF 1  
Share:

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

IDADI YA WANAOTEMBELEA BLOG HII

Blog Archive

Recent Posts

Fashion

3/Fashion/big-col-right

Recent Posts

Header Ads

Followers

Powered By Blogger

Tags

Maoni

3/recent-comments

WASILIANA NASI

Popular Posts

Labels

Blog Archive

Blogger templates