Mbio hizo zilishuhudia mwanariadha wa Tanzania Fabiola William (32),ameibuka mshindi wa kilomita 42 (Full Marathon) katika mbio za Kilimanjaro Marathon zilizofanyika jana mjini hapa na kujinyakulia Sh milioni 4 baada ya kutumia 2:49:51.

Nafasi ya pili ilichukuliwa na Rosaline David (Kenya) aliyetumia 2:50:39 na kujinyakulia Sh milioni mbili wakati nafasi ya tatu ilichukuliwa na Joan Cherop (Kenya) alitumia 2:50:44 na kujinyakulia Sh milioni moja.
Kwa upande wa Half Marathon Kiloimita 21 wanaume, Ismael Juma (Tanzania), aliibuka mshindi baada ya kutumia 1:03:05 na kujinyakulia Sh milioni 2 huku nafasi ya pili ikienda kwa Emmanuel Giniki (Tanzania), aliyetumia 1:03:15 na nafasi ya tatu ilikwenda kwa Theotil Joseph (Tanzania), aliyetumia 1:03:25.
Akizungumza katika mbio hizo, mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani, Mathias Chikawe, aliwapongeza waandaaji wa tukio hilo la aina yake.
0 comments:
Post a Comment