Pages

Monday, 9 March 2015

FA CUP ARSENAL YAIUA MANCHESTER UNITED OLD TRAFFOD YASHINDA 2-1 NA KUTINGA NUSU FAINALI


Arsenal jana imefuta uteja kwa Manchester united baada ya kuibabua 2-1 Dan Welbeck, ambae aliuzwa na Manchester United kwa Arsenal mwanzoni mwa Msimu, amerudi Old Trafford kwa mara ya kwanza na kufunga Bao la pili na la ushindi wakati Arsenal inaiishinda Man United 2-1 kwenye Robo Fainali ya FA CUP.
Arsenal walitangulia kufunga kwa Bao la Dakika ya 25 la Nacho Monreal na Wayne Rooney kusawazisha Dakika ya 29 lakini Welbeck kuipa ushindi Arsenal katika Dakika ya 61.
Man United walimaliza Mechi hii Mtu 10 baada ya Angel Di Maria kulambwa Kadi za Njano mbili na kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu.
Usiku wa jana ulikuwa mwema kwa Arsenal ambao wameendelea kutetea vyema Kombe la FA CUP ambalo wao ni Mabingwa Watetezi na pia wamekuwa wakiteswa na Man United kwa kufungwa Mechi 11 kati ya 15 zilizopita.
Pia kwenye Droo ya Nusu Fainali ya FA CUP, iliyofanyika mara baada ya Mechi hii, Arsenal watacheza na Mshindi kati ya Bradford City au Reading ambao Juzi walitoka 0-0 kwenye Mechi yao ya Robo Fainali.
Nusu Fainali nyingine itakuwa kati ya Mshindi wa Liverpool na Blackburn Rovers, ambao nao walitoka 0-0, dhidi ya Aston Villa.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

IDADI YA WANAOTEMBELEA BLOG HII

Blog Archive

Recent Posts

Fashion

3/Fashion/big-col-right

Recent Posts

Header Ads

Followers

Powered By Blogger

Tags

Maoni

3/recent-comments

WASILIANA NASI

Popular Posts

Labels

Blog Archive

Blogger templates