Raisi
wa shirikisho la soka nchini Jamal Malinzi amefuta michezo yote ya ligi
kuu ya Tanzania bara iliyokuwa ichezwe hapo kesho katika viwanja vya
Taifa na Mkwakwani.
Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya kimataifa Yanga, kesho
walikuwa na mchezo dhidi ya JKT Ruvu katika uwanja wa Taifa, wakati
jumapili watakuwa na kibarua cha kuiwakilisha nchi katika kombe la
shirikisho dhidi ya FC Platnum.
Mchezo mwingine wa kesho ulikuwa ni kati ya Azam fc na Mgambo shooting katika uwanja wa Mkwakwani.
Kuhairishwa kwa michezo hiyo kuna ipa muda zaidi wa yanga kujiandaa
na mchezo wa kimataifa hapo jumapili, wakati azam fc wakielekeza
maandalizi yao kwa mchezo dhidi ya Ndanda FC jumamosi.
Monday, 9 March 2015
Home »
» MICHEZO YA KESHO YA LIGI KUU YA VODACOM YAFUTWA NA TFF HAKUNA MECHI
0 comments:
Post a Comment