BEKI wa Manchester United Jonny Evans amefungiwa mechi 6 na FA, Chama cha Soka England, la kumtemeana mate Fowadi wa Newcastle Papiss Cisse ambaye nae amefungiwa mechi 7 wakati wa Mechi ya Ligi Kuu England Jumatano iliyopita Uwanjani St James Park
ambayo united walishinda 1-0.
Kwa mujibu wa taarifa zilizonifikia hivi punde Tayari Papiss Cisse amekiri Shitaka hilo hilo la kumtemea mate Evans na amefungiwa Mechi 6 pamoja na moja ya ziada kwa vile Msimu huu tayari alishawahi kuwa Kifungoni.
Tukio hilo, ambalo halikuonwa na Refa, lilitokea Dakika ya 38 ya Gemu hiyo ambapo Evans alimvaa Cisse alieanguka chini na Evans kuonekana akitema mate upande wa Cisse ambae baada ya kuinuka alimtemea mate Evans shingoni.
Kabla ya FA kutangaza kufungua Mashitaka dhidi yao, Papiss Cisse alimwomba radhi Jonny Evans pamoja na Wadau wa Soka lakini , Evans alikanusha kukusudia kumtemea mate Cisse na kudai si hulka yake kufanya kitendo cha aina hiyo.
0 comments:
Post a Comment