Mshambuliaji wa kilabu ya Swansea
Bafetimbi Gomis alianguka na kuzimia uwanjani, ikiwa ni kisa cha hivi
karibuni cha mchezaji huyo ambaye amekuwa akikabiliwa na tatizo hilo
mara kwa mara.
Swansea ilikuwa ikimenyana na kilabu ya Totenham
Hospurs wakati wa tukio hilo na kusababisha mchezo kusimamishwa kwa
dakika tano ili madaktari kumuhudumia mchezaji huyo.Mechi hiyo ilikamilika ikiwa Totenham imeibuka kidedea kwa mabao 3-2
Raia huyo wa Ufaransa amekabiliwa na tatizo hilo mara kadhaa ikiwemo mara tatu alipokuwa akiichezea kilabu ya Lyon mnamo mwaka 2009 na chengine wakati alipokuwa katika kambi ya mazoezi na, wasiwasi uliwazonga wachezaji wenzake katikati ya uwanja alipokuwa akipokea matibabu.
0 comments:
Post a Comment