Jose Mourinho anaamini Chelsea wapo njiani kutwaa Ubingwa baada ya Jana kupigana na kushinda 3-2 huko KC Stadium walipocheza na Hull City.
Ushindi huo, uliopatikana kwa Bao la 3 la Loic Remy baada ya Chelsea kuongoza 2-0 na Hull kurudisha na Gemu kuwa 2-2, umewafanya Chelsea wawe Pointi 6 mbele ya Man City huku wakiwa na Gemu 1 mkononi na sasa njia inazidi kufunguka kwao kutwaa Ubingwa wao wa kwanza tangu 2010.
Mourinho amesema: “Mbio za Ubingwa zilipaswa kuwa zimekwisha. Kwa hali ya kawaida, Chelsea walitakiwa wawe Pointi 8, 10, 12 au zaidi mbele. Lakini Soka haitabiriki na sasa tupo Pointi 6 mbele na ni nafasi safi kupita tulipokuwepo. Ninajiamini na naamini Wachezaji wangu!”
0 comments:
Post a Comment