Pages

Sunday, 1 March 2015

LEO NI FAINALI CAPITAL ONE CUP CHELSEA VS TOTTENHAM NANI KUBEBA KOMBE?

HII ni mara ya pili kwa Chelsea kukutana na Tottenham kwenye Fainali ya Kombe la Ligi, Capital One Cup, mara ya kwanza ikiwa 2008 na Spurs kushinda na safari hii wanakutana tena Jumapili Uwanjani Wembley Jijini London wakitoka tu kwenye Mechi ya Ligi ambayo Chelsea walibamizwa Bao 5-3 huku Harry Kane aking’ara kwa kupiga Bao 2.
Mwaka 2008, Bao la Kichwa la Dakika za Nyongeza 30 la Jonathan Woodgate liliwapa Kombe hili lakini safari hii Spurs wanae Chipukizi moto Harry Kane mwenye Miaka 21, ambae Mwezi uliopita aliitesa sana Chelsea.
Chelsea watacheza Fainali hii bila ya Kiungo wao Nemanya Matic ambae amefungiwa Mechi 2 na FA baada ya Kadi Nyekundu.
NINI MAMENEJA WANASEMA:
CHELSEA - Jose Mourinho: "Ni Fainali ambayo inabidi tucheze na Fainali ambayo tunapaswa kushinda!”
TOTTENHAM - Mauricio Pochettino: "Wachezaji wanapaswa kujua mie ndie Bosi na nachagua Kikosi. Ni kweli hii ni Fainali na Gemu muhimu lakini Wachezaji wanapaswa kuheshimu uteuzi wangu!”
Mara ya mwisho kwa Chelsea na Tottenham kukutana ni Mwezi uliopita Januari Mosi Uwanjani White Hart Lane kwenye Mechi ya Ligi Kuu England na Tottenham Hotspur wakaibamiza Chelsea Bao 5-3 na Straika hatari na Chipukizi wa Tottenham, Harry Kane, aliiongoza Spurs kwa kupiga Bao 2 na kutengeneza nyingine.
Tottenham wametinga Fainali baada ya kuitoa Sheffield United kwa Jumla ya Mabao 3-2 kwa kushinda Mechi ya Kwanza wakiwa kwao White Hart Lane 1-0 kwa Bao la Penati ya Andros Townsend na kisha kutoka Sare 2-2 katika Marudiano Nyumbani kwa Sheffield United.
Nao Chelsea walitinga Fainali baada ya kuifunga Liverpool 1-0 kwa Bao la Dakika za Nyongeza 30 la Branislav Ivanovic wakiwa Stamford Bridge baada ya Sare ya 1-1 katika Mechi ya Kwanza huko Anfield na kutinga Fainali kwa Jumla ya Mabao 2-1.
CHANZO :SOKA IN TANZANIA
Share:

2 comments:

  1. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  2. Binafsi nawapa nafasi Spurs kwa sababu 2.
    1. Wanataka kurejesha furaha iliyopotea ya kushangilia kikombe
    2. Hawana pressure saaana hasa ukizingatia hawapo kwenye racê
    za kuchukuà EPL due to gap na vinara Chelsea.
    Kwa upande wa Chelsea watàcheza kwa temper ya hali ya juu hasà ukizingatia kauli ya Jose itawafanya wawe watumwa so hii itawafanya wasicheze kàma tulivyowazoea.
    Anything can happen lakini kura yangu iko Spurs. Mwl Chimbenga from Tangazo.

    ReplyDelete

Powered by Blogger.

IDADI YA WANAOTEMBELEA BLOG HII

Blog Archive

Recent Posts

Fashion

3/Fashion/big-col-right

Recent Posts

Header Ads

Followers

Powered By Blogger

Tags

Maoni

3/recent-comments

WASILIANA NASI

Popular Posts

Labels

Blog Archive

Blogger templates