Baada ya kujihakikishia kusonga mbele katika michuano ya kimataifa vinara wa ligi kuu ya Tanzania bara Yanga sasa watacheza na Platinum FC ya Zimbabwe katika kombe la shirikisho baada ya ijumaa Yanga kuwatoa BDF XI nao Platinum FC wakiiondosha Sofapaka ya Kenya jana.
Platinum jana waliwafunga Sofapaka ya Kenya goli 2-1 na kupelekea kuiondosha kwa jumla ya goli 4-2, baada ya mchezo wa awali uliochezwa Kenya kushuhudia Platinum wakiibuka na ushindi kama huo wa jana.
Yanga wao wameitoa BDF XI ya Botswana kwa jumla ya magoli 3-2 na kufanikiwa kutinga katika hatua hiyo.
Sunday, 1 March 2015
Home »
» YANGA KUCHEZA NA PLATINUM FC YA ZIMBABWE HATUA YA 32 BORA KOMBE LA SHIRIKISHO
0 comments:
Post a Comment