Ligi Kuu England itaendelea Jumanne na Jumatano kwa Timu zote 20 kucheza Mechi.
Hapo Jumanne Machi 3 zipo Mechi 3 kuanzia Villa Park ambako Aston Villa watacheza na West Bromwich Albion wakati Hull City wataivaa Sunderland na Southampton kucheza na Crystal Palace.

Jumatano zipo Mechi 7 ambapo Mabingwa Watetezi Manchester City watakuwa kwao kucheza na Leicester City huku Jirani zao, Man United, wakiwa Ugenini huko Saint James Park kucheza na Newcastle.
Nao Vinara wa Ligi, Chelsea, watakuwa Ugenini huko Upton Park kucheza na West Ham na pia Arsenal kuwa Ugenini kuivaa QPR wakati Liverpool wako Nyumbani kucheza na Burnley
Hapo Gunners hakuna wa kutuzuia tutampiga mtu zaidi ya goli 2
ReplyDelete