Azam FC imetangaza kumfukuza kazi Kocha Joseph Omog raia wa
Cameroon.
Pamoja na Omog, Msaidizi wake, Ibrahim Shikanda ametimuliwa na
mikoba amepewa George Best Nsimbe raia wa Uganda ambaye ni msaidizi wake namba
moja.
Best ambaye ameanza kazi Azam FC msimu uliopita, sasa ndiye
ataongoza jahazi.
Azam FC ilianza kwa kushinda 2-0 jijini Dar lakini ikakubali kipigo cha mabao 3-0 jijini Kharthoum.
Omog ndiye aliyeipa Azam FC ubingwa wake wa kwanza wa Ligi Kuu Bara na ushindi wake wa kwanza katika Ligi ya Mabingwa Afrika .
0 comments:
Post a Comment