MAN CITY 2-0 LEICESTER CITY
Bao 2 za David Silva na James Milner, moja kila Kipindi zimewapa ushindi wa Bao 2-0 Mabingwa Watetezi Man City waliokuwa wakicheza kwao dhidi ya Leicester City.
Ushindi huu umewabakisha City Nafasi ya Pili wakiwa Pointi 5 nyuma ya Vinara Chelsea.
NEWCASTLE 0 MAN UNITED 1
Bao la Dakika ya 89 la Ashley Young limewapa ushindi wa Bao 1-0 Manchester United waliokuwa wakicheza Ugenini huko Saint James Park dhidi ya Newcastle.
Bao hilo lilitokana na makosa ya Kipa wa Newcastle Tim Krul kushindwa kuiondoa Pasi aliyopewa na Mchezaji wake Mehdi Abeid na badala yake kumruhusu Young kuunasa Mpira na kufunga vizuri.
Ushindi huu umewabakiza Man United Nafasi ya 4 wakiwa Pointi 1 nyuma ya Arsenal ambao wako Nafasi ya 3.
QPR 1 ARSENAL 2
Bao za Kipindi cha Pili za Olivier Giroud na Alexis Sanchez zimewapa Arsenal ushindi wa Bao 2-1 walipocheza na QPR Ugenini huko Loftus Road.
QPR walipata Bao lao moja wakati Gemu ikiwa 2-0 katika Dakika ya 82 kupitia Charlie Austin.
Ushindi huu umewabakisha Arsenal Nafasi ya 3 wakiwa Pointi 4 nyuma ya Timu ya 3 Man City na 9 nyuma ya Vinara Chelsea.
WEST HAM 0 CHELSEA 1
Vinara wa Ligi Kuu England, Chelsea, wamebakia Pointi 5 mbele ya Timu ya Pili Man City huku wakiwa wamecheza Mechi 1 pungufu baada ya kuifunga West Ham Bao 1-0 Ugenini huko Upton Park.
Bao la ushindi la Chelsea lilifungwa na Eden Hazard katika Dakika ya 22 kufuatia Krosi ya Ramires.
MATOKEO MENGINE
Stoke 2 Everton 0
Tottenham 3 Swansea 2
Liverpool 2 Burnley 0
MSIMAMO:

0 comments:
Post a Comment