Pages

Thursday, 5 March 2015

KUELEKEA MECHI YA WATANI: COUTINHO KUIKOSA MECHI YA SIMBA NA YANGA

Kiungo wa Yanga  Andrey Coutinho imethibitishwa kwamba hatocheza mechi dhidi ya Simba hapo Machi 8.
Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm amesema alimuachia daktari afanye kazi yake ili kuangalia kama Coutinho atacheza mechi ya Jumapili.
“Kwa hali ilivyo, inaonekana imeshindikana. Hivyo ataendelea na matibabu pia mazoezi rahisi.
“Baada ya mechi yetu na Simba, Jumapili tutaona hali yake inaendeleaje,” alisema Pluijm.
“Zile mechi za Mbeya zilikuwa ngumu sana, mchezaji yoyote angeweza kuumia, hivyo si jambo geni na tuna wachezaji wengine watachukua nafasi yake kama ilivyokuwa kule Botswana.”
Yanga ilisafiri kwenda Botswana kuivaa BDF katika mechi ya pili ya Kombe la Shirikisho bila ya Mbrazili huyo. Ilipoteza kwa mabao 2-1, lakini ikasonga mbele kwa jumla ya mabao 3-2 baada ya ushindi wake wa 2-0 katika mechi ya kwanza jijini Dar.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

IDADI YA WANAOTEMBELEA BLOG HII

Blog Archive

Recent Posts

Fashion

3/Fashion/big-col-right

Recent Posts

Header Ads

Followers

Powered By Blogger

Tags

Maoni

3/recent-comments

WASILIANA NASI

Popular Posts

Labels

Blog Archive

Blogger templates