Ndanda Fc ya mtwara imeitandika timu ya ruvu shooting magoli 2-1 katika mchezo uliochezwa uwanja wa mabatini mkoani pwani magoli ya ndanda yamefungwa na Jacob Masawe na omega Seme kwa matokeo hayo Ndanda imepanda hadi nafasi ya 7 ikiwa na pointi 22
Huko Manungu baada ya wakati mgumu wa kufungwa mfululizo hatimaye Mtibwa Sugar imerejea katika listi ya ushindi.
Mtibwa Sugar imeifunga Polisi Moro kwa mabao 2-1 katika mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Manungu mjini Turiani.
Polisi ndiyo walikuwa wa kwanza kuandika bao kupitia Said Bahanuzi katika dakika ya 41 likadumu hadi mapumziko.
Lakini kipindi cha pili kilikuwa cha Mtibwa Sugar ambayo ilifunga mabao yake kupitia Ali Shomari katika dakika ya 53 na Said Mkopi akamaliza kazi katika dakika ya 79.
Kwa ushindi huo, sasa Mtibwa Sugar imefanikiwa kufikisha pointi 22.
Katika uwanja wa chamazi coplex timu za Prison na Ruvu jkt stars zimetoka sare ya bila kufungana
0 comments:
Post a Comment