Wawakilishi wa Tanzania katika kombe la
shirikisho Yanga wametangaza nia ya kugomea mchezo dhidi ya ligi kuu ya
vodacom dhidi ya JKT Ruvu ulipangwa kuchezwa marchi 11 mwaka huu katika
uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Mkuu wa kitengo cha habari wa yanga
Jerry Muro, akizungumzaq na vyombo vya habari leo amesema kuwa yanga
hawataingiza timu uwanjani marchi 11, kama mchezo huo hauto chezwa
kesho, kama ratiba ya awali ilivyokuwa inaonyesha.
Jerry alisema kuwa mabadiliko hayo ya
ratiba uongozi wa yanga hawaya jui kwa kuwa hawana taarifa maalum toka
kwa bodi ya ligi juu ya mabadiliko hayo ya ratiba.
Muro amesema bodi ya ligi imeonyesha
kwamba haitaki Yanga ifanikiwe katika kampeni zao za kombe la Shirikisho
kwa kuitaka kuucheza mchezo huo Machi 11 ikiwa ni siku tatu kabla ya
kushuka katika Uwanja wa Taifa kucheza na Plutinum ya Zimbabwe.
"Tumewaambia
tangu jana kama wameufuta mchezo wa kesho na badala yake wakaupeleka
Machi 11 Yanga hatutakuja uwanjani kwakuwa huo sio uzalendo hatuwezi
kuacha maandalizi ya mechi yetu ya kimataifa kuangalia mechi ya ligi."
aliongeza Muro
Wakati Muro akisema hayo kaimu ofisa
mtandaji Mkuu wa bodi ya ligi Fatma Abdallah amesema kuwa yanga
walitumia kwa njia ya Email mabadiliko hayo ya ratiba, toka februari 15
mwaka huu. Fatma Abdallah alisema hayo pale alipo kuwa anahojiwa na
kituo cha redio nchini.
Mabadiliko ya ratiba msimu huu wa ligi
kuu ya vodacom yamekuwa yakitokea mara kwa mara, na kupelekea kuharibu
mipango ya timu shiriki kutokana na mabadiliko hayo.
Wednesday, 4 March 2015
Home »
» YANGA KUTISHIA KUGOMEA MECHI NI MKWARA TU TAARIFA WANAYO KWA MUJIBU WA BODI YA LIGI
0 comments:
Post a Comment