Pages

Wednesday, 4 March 2015

LIGI KUU UINGEREZA JANA DABI YA MIDLANDS ASTON VILLA USHINDI LEO MECHI 7 DIMBANI

LIGI KUU ENGLAND iliendelea kwa Mechi 3 Jana Usiku na Dabi ya Midlands ilipigwa Uwanjani Villa Park na Meneja Tim Sherwood kupata ushindi wake wa kwanza tangu ateuliwe Meneja mpya baada ya Penati ya Dakika za Majeruhi ya Straika wake Christian Benteke kuwapa Bao la ushindi walipoichapa West Bromwich Albion Bao 2-1.
Penati hiyo ilitolewa baada ya Kipa Ben Forster kuutema Mpira na kisha kumwangusha Mathew Lowton wakatia akiwania kuokoa.
Villa walitangulia kufunga kwa Bao la Gabriel Agbonlahor lakini WBA wakasawazisha kwa Bao la Saido Berahino.
Ushindi huu umeing’oa Villa toka mkiani na kuipandisha sehemu salamu wakiwa Nafasi ya 17.
Katika Mechi nyingine mbili za Ligi zilizochezwa Jana, Hull City na Sunderland zilitoka Sare 1-1 na Southampton kuifunga Crystal Palace Bao 1-0.
Ligi Kuu England itaendelea tena Usiku huu kwa Mechi 7.
MECHI ZA LEO
2245 Man City v Leicester 
2245 Newcastle v Man United     
2245 QPR v Arsenal          
2245 Stoke v Everton       
2245 Tottenham v Swansea        
2245 West Ham v Chelsea
2300 Liverpool v Burnley            


Share:

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

IDADI YA WANAOTEMBELEA BLOG HII

Blog Archive

Recent Posts

Fashion

3/Fashion/big-col-right

Recent Posts

Header Ads

Followers

Powered By Blogger

Tags

Maoni

3/recent-comments

WASILIANA NASI

Popular Posts

Labels

Blog Archive

Blogger templates