Pages

Tuesday, 3 March 2015

MCHEZAJI WA SUNDERLAND ADAM JOHNSON AKAMATWA NA POLISI KISA KUFANYA MAPENZI NA BINTI WA MIAKA 15

Sunderland imemsimamisha Winga wao Adam Johnson baada ya kukamatwa na Polisi kwa tuhuma za kufanya ngono na Binti wa chini ya Umri halali.
Baada ya Polisi kutoa Taarifa kuwa Mtu wa Miaka 27 alikamatwa kwa tuhuma za kufanya ngono na Binti wa chini ya Miaka 16, Magazeti mengi huko Uingereza yaimtuhumu Adam Johnson kuwa ndie Mtuhumiwa kwa kutenda kitendo hicho na Binti wa Miaka 15.
Mpenzi wa winga Adam Johnson amesisitiza atamuunga mkono mpenzi wake katika kesi ya inayomkabili 
Johnson anayekipiga Sunderland amekamatwa juzi na tayari Sunderland imetangaza kumsimamisha kutokana na suala hilo.
Johnson ambae sasa yupo huru baada ya Polisi kumuachia kwa dhamana, alianza Soka lake huko Middlesbrough na kisha kujiunga na Manchester City.
Alihamia Sunderland Mwaka 2012 kwa Dau la Pauni Milioni 1o lakini ameshindwa kuonyesha cheche zake za huko nyuma.
Hata hivyo, Mashabiki wa Sunderland wanamthamini sana kwani kwenye Dabi yao na Mpinzani wao mkuu, Newcastle, Johnson amekuwa akipiga Bao muhimu likiwemo Bao la ushindi la Dakika za mwishoni huko St James' Park hapo Desemba 21 Mwaka Jana.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

IDADI YA WANAOTEMBELEA BLOG HII

Blog Archive

Recent Posts

Fashion

3/Fashion/big-col-right

Recent Posts

Header Ads

Followers

Powered By Blogger

Tags

Maoni

3/recent-comments

WASILIANA NASI

Popular Posts

Labels

Blog Archive

Blogger templates