Pages

Tuesday, 3 March 2015

CHAMA CHA SOKA UINGEREZA KIMEFUTA KADI NYEKUNDU YA WEST BROWN LEO ATAKUWA UWANJANI SUNDERLAND IKIWAVAA HULL CITY

FA, Chama cha Soka England, kimeifuta Kadi Nyekundu aliyopewa Beki wa Sunderland Jumamosi iliyopita walipofungwa 2-0 na Manchester United Uwanjani Old Trafford kwenye Mechi ya Ligi Kuu England.
Wes Brown alitolewa katika Dakika ya 64 licha ya kuonyeshwa wazi kuwa ni mwenzake John O'Shea ndie aliemchezea Faulo Fowadi wa Man United, Falcao.
Sunderland walikata Rufaa kupinga Kadi hiyo na sasa Jopo Huru la FA limeamua Kadi hiyo haikustahili kwa Wes Brown na kufutwa.
Uamuzi huo wa kufuta Kadi Nyekundu kwa Brown pia unalimnda John O'Shea ambae hakuhamishiwa Kadi hiyo na sasa wote wawili wako huru kuichezea Sunderland watakapokuwa Ugenini kuivaa Hull City kwenye Mechi ya Ligi Kuu England.
Meneja wa Sunderland, Gus Poyet, amepokea habari hizi kwa kusifia na kushukuru ukweli wa Refa Roger East, PGMOL [Bodi ya Marefa wa Kulipwa England] na Ligi Kuu England kwa kulimaliza suala hili ipasavywo.
Tukio la Kadi Nyekundu kwa Wes Brown pia lilizaa Penati ambayo Nahodha wa Man United, Wayne Rooney, alifunga na baadae kuongeza Bao la Pili.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

IDADI YA WANAOTEMBELEA BLOG HII

Blog Archive

Recent Posts

Fashion

3/Fashion/big-col-right

Recent Posts

Header Ads

Followers

Powered By Blogger

Tags

Maoni

3/recent-comments

WASILIANA NASI

Popular Posts

Labels

Blog Archive

Blogger templates