MARUDIANO ya Kombe la Mfalme huko Spain, Copa del Rey, yatafanyika Jumatano Machi 4 huku Vigogo Barcelona wakiwa kwenye mguu mzuri kushinda Mechi hii.
Barcelona walianza vyema Mechi ya Kwanza ya Nusu Fainali walipoichapa Villareal 3-1 Uwanjani Nou Camp na Timu hizi sasa zitarudiana Nyumbani kwa Villareal Estadio El Madrigal Mjini Villareal.
Juzi Villareal walichezesha Timu hafifu walipotoka Sare 1-1 na Real Madrid huko Santiago Bernabeu kwenye Mechi ya La Liga ili kutilia mkazo Marudiano haya na Barcelona.
Mechi nyingine ya Nusu Fainali ambayo nayo itachezwa Jumatano itakuwa huko Estadi Cornella-El Prat, Mjini Barcelona kati ya Wenyeji Espanyol na Athletic Bilbao.
Katika Mechi ya Kwanza iliyochezwa Nyumbani kwa Bilbao, Timu hizi zilitoka Sare ya 1-1.
Washindi wa Nusu Fainali hizi watacheza Fainali hapo Mei 30 kwenye Uwanja ambao bado haujathibitishwa.
0 comments:
Post a Comment