LIGI KUU VODACOM inaendelea Jumatano kwa Mechi 3 na Jumamosi Mechi 3 pia lakini Macho na Masikio ya Washabiki wote ni ile Bigi Mechi ya Jumapili ambayo ni Dabi ya Kariakoo kati ya Miamba ya Soka Tanzania, Simba, na Watani zao Yanga, itayochezwa Jijini Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Taifa.
Katika Mechi yao ya kwanza ya Msimu huu kwenye Ligi Kuu Vodacom, Timu hizi zilitoka Sare ya 0-0 lakini kama kawaida licha tu ya kuwa ni moja tu ya Mechi zao za Ligi, Yanga na Simba huchukulia Dabi hii kwa uzito mkubwa hata kama iwe Mechi aina ya gani.
Kwa hali hiyo kila Timu imeandaa maandaliza kabambe kwa Simba kufanya Mkutano Mkuu wa Wanachama Jumapili ili kuwekana sawa na kisha kuikimbiza Timu yao Kambini huko Visiwani Zanzibar ambako watakuwa chini ya Kocha wao kutoka Serbia, Goran Kapunovic.
Simba wamelekea kwenye Dabi hii wakitoka kwenye ushindi mnono wa Ligi walipoitwanga Tanzania Prisons Bao 5-0 Jumamosi iliyopita.
Yanga nao baada ya kutoka huko Gaborone, Botswana ambako Wikiendi hii iliyopita walifanikiwa kufuzu kutinga Raundi ya Kwanza ya Mashindano ya CAF ya Kombe la Shirikisho baada ya kuitoa BDF XI kwa Jumla ya Mabao 3-2.
Yanga walishinda Mechi ya Kwanza 2-0 na kufungwa Mechi ya Pili 2-1.
Mara baada ya kutua Jijini Dar es Salaam, Yanga chini ya Kocha wao kutoka Uholanzi, Hans van der Pluijm akisaidiwa na Charles Boniface Mkwasa, walielekea moja kwa moja Bagamoyo kupiga Kambi kwa ajili ya Dabi hii.
Yanga hivi sasa ndio Vinara wa Ligi Kuu Vodacom wakiwa na Pointi 31 kwa Mechi 15 wakifuatiwa na Azam FC wenye Pointi 27 kwa Mechi 15 kisha Kagera Sugar waliocheza Mechi 17 na wana Pointi 24 na ya 4 ni Simba wenye Pointi 23 kwaMechi 16.








0 comments:
Post a Comment