Mechi ya Simba na
Yanga imekuwa ikivuta hisia za mashabiki kwa nchi nzima na mara nyingi zimekuwa
na changamoto nyingi baada ya kumalizika.
Taarifa za uhakika
kutoka kwenye kamati ya waamuzi, zinasema kuwa Martin Saanya ambaye mashabiki
wa Yanga haziivi, ndiye amepewa ‘rungu’ katika kesi hiyo, kama mwamuzi wa kati
akisaidiwa na Idd Lila wa Dar es Salaam pamoja na Florentina Zabrone, kutoka
Dodoma, wakati Israel Nkongo akisimama kama mwamuzi wa mezani.
Saanya bado
mashabiki wa Yanga hawana imani naye tangu ashutumiwe kuwafanyia ndivyo sivyo katika mchezo
na Coastal Union msimu wa 2012/13 , baada ya kuipa Coastal penalti dakika za
mwisho kabisa, hali iliyosababisha vurugu kubwa na uharibifu wa mali.
0 comments:
Post a Comment