Liverpool Leo wapo Ewood Park kurudiana na Blackburn Rovers katika Robo Fainali ya FA Cup baada kutoka 0-0 Mwezi uliopita huko Anfield.
Liverpool, ambao hawajatwaa Kombe tangu 2012 walipotwaa Kombe la Ligi wakiwa chini ya Kenny Dalglish, wataingia kwenye Mechi hii wakiwakosa Wachezaji Watatu ambao wapo Kifungoni na hao ni Nahodha Steven Gerrard, Martin Skrtel na Emre Can.
Baada kutansikwa 4-1 na Arsenal Jumamosi na kupoteza mwelekeo wa kufuzu kwenye 4 Bora za Ligi Kuu England, hii ni nafasi safi kwa Liverpool kung'arisha Msimu wao.
Nao Blackburn Rovers, ambao wako Nafasi ya 10 kwenye Ligi ya Championship ambayo iko chini tu ya Ligi Kuu England, walizibwaga Timu za Ligi Kuu Swansea na Stoke hapo hapo Uwanjani kwao Ewood Park na kufika hatua hii ya FA CUP.
Lakini safari hii watawakosa Wachezaji wao Watatu ambao ni Majeruhi na hao ni Jason Lowe, Shane Duffy na Chris Taylor.
Mshindi wa Mechi hii atacheza Nusu Fainali Uwanjani Wembley dhidi ya Aston Villa.
0 comments:
Post a Comment