Pages

Wednesday, 1 April 2015

LIGI KUU KUENDELEA WEEKEND HII SIMBA KTUPA KARATA YAKE NA KAGERA MTWARA BIG MECHI NDANDA NA MBEYA CITY


Ligi Kuu Vodacom itaendelea weekend hii mechi 5 timu 10  kukipiga kutafuta pointi 3 muhimu
Viwanja vitano kuwaka moto Manungu, Mkwakwani, Mabatini, Nangwanda na Kambarage.
Simba, ambao wako Nafasi ya 3, watakuwa Wageni wa Kagera Sugar huko Kambarage Jijini Shinyanga badala ya Kaitaba, Bukoba ambayo iko kwenye ukarabati.
Kocha Mkuu wa Simba, Goran Kopunovic amesisitiza hata kama iko ugenini, Simba inalazimisha kushinda dhidi ya Kagera Sugar

“Tunajua Kagera ni timu nzuri, lakini katika ligi hii kumbuka hakuna timu dhaifu Ila kuna timu kongwe na timu imara zaidi. Sisi tunachoangalia ni kufanya vizuri na kushinda.

“Tutaanza safari ya kwenda Kagera tukiwa na lengo moja tu, kushinda mechi na kurudi na pointi tatu,” alisisitiza MSerbia huyo.
Kagera Sugar wako Nafasi ya 4 wakiwa Pointi 7 nyuma ya Simba lakini wao wamecheza Mechi 1 pungufu.
Huko Manungu, Morogoro, Mtibwa Sugar, ambao wako Nafasi ya 8, wataivaa Stand United wanaoshikilia Nafasi ya 13 ikiwa ni nafasi moja tu juu ya Timu ya Mkiani Tanzania Prisons ambayo itacheza Mkwakwani, Tanga na Coastal Union wanaokamata Nafasi ya 5.
Huko Mabatini, Mlandizi ni vita ya Timu za Ruvu wakati Ruvu Shooting watakapoikaribisha Ruvu JKT ambayo iko Nafasi ya 6 ikitenganishwa na Pointi 1 tu na Ruvu Shooting walio Nafasi ya 10.
Huko Nangwanda, Mtwara, Ndanda FC, walio Nafasi ya 11 wataikaribisha Mbeya City walio Nafasi ya 9 lakini Timu zote zina Pointi sawa ila zinatenganishwa na Ubora wa Magoli
Share:

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

IDADI YA WANAOTEMBELEA BLOG HII

Blog Archive

Recent Posts

Fashion

3/Fashion/big-col-right

Recent Posts

Header Ads

Followers

Powered By Blogger

Tags

Maoni

3/recent-comments

WASILIANA NASI

Popular Posts

Labels

Blog Archive

Blogger templates