Vinara wa Ligi Kuu England Chelsea wameendelea kupeperuka kileleni mwa Ligi baada ya kuifunga Stoke City Bao 2-1 Uwanjani Stamford Bridge.
Ushindi huu umeipa Chelsea Pointi 70 kwa Mechi 30 wakifuatiwa na Arsenal wenye Pointi 63 kwa Mechi 31 kisha Man United wenye Pointi 62 kwa Mechi 31 na Man City wako Nafasi ya 4 wakiwa na Pointi 61 kwa Mechi 30.
Mabao ya Mechi ya Leo yalifungwa na Eden Hazard kwa Penati ya Dakika ya 39 baada Cesc Fabregas kuchezewa faulo lakini Stoke walisawazisha Dakika ya 44 kwa Bao zuri sana la Charlie Adam alipomfuma Kipa wa Chelsea Courtois akiwa ametoka Golini na yeye kurusha kombora la juu kutoka Mita 65, upande wa Uwanja wa Stoke, na kutinga wavuni.
Makosa makubwa ya Kipa wa Stoke Begovic aliporusha Mpira kumpasia Beki wake na Mpira huo kunaswa na Willian na kisha kupelekewa Remy aliefunga Bao la Pili na ushindi kwa Chelsea.
MATOKEO
Arsenal 4 Liverpool 1
Everton 1 Southampton 0
Leicester 2 West Ham 1
Man United 3 Aston Villa 1
Swansea 3 Hull 1
West Brom 1 QPR 4
1930 Chelsea v Stoke
MECHI ZA LEO
Jumapili Aprili 5
1530 Burnley v Tottenham
1800 Sunderland v Newcastle
0 comments:
Post a Comment